ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 12, 2022

HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAFUKUZWA UANACHAMA CHADEMA


Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limeunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho wa kuwafukuza uanachama aliteuliwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama hicho (BAWACHA) Bi. Halima Halima na wenzake 18 kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge wa viti maalumu bila kupata baraka za chama hicho.
Pamoja na Halima Mdee, wengine waliofukuzwa uanachama ni Grace Tendega, Esther Matiko, Jesca Kishoa, Ester Bulaya, Anatropia Theonest, Cecilia Pareso na Agnes Kaiza.

Wengine ni Nuzrat Shaban Hanje, Stella Simon Fiao, Hawa Mwaifunga, Felista Deogratius Njau, Nagenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunt Majala, Tunza Malapo, Asna Mohamed, Salome Makamba na Conjesta Rwamulaza.

Uamuzi wa kuwafukuza uanachama ulifanyika kwa wajumbe hao WA Baraza Kuu kupiga Kura ambapo Kura za Wajumbe 413 dawa na asilimia 97.6% ya wajumbe wote 423 waliopiga Kura, huku Wajumbe 5 sawa na asilimia 1.2% hawakukubaliana na uamuzi wa Kamati Kuu WA kuwafukuza uanachama na Wajumbe 5 sawa na asilimia 1.2% hawakufungamana na upande wote.

“Kilichofanyika pale wapiga kura hawakuwa huru ni uhuni naweza kusema kilichotokea ni uhuni wa kiwango Cha juu, nitaongeza siku nyingine Mimi na wenzangu, sasa hivi sio muda muafaka na Mimi ni CHADEMA na nitaendelea kuwa CHADEMA” Alisema Halima Mdee mbele ya Waandishi wa habari mara baada ya uamuzi huo.

Halima Mdee na wenzako waliapishwa kuwa wabunge WA Viti maalum kutoka CHADEMA Novemba 24, 2020, hatua iliyopingwa vikali na Wakuu wa CHADEMA.

No comments: