ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 11, 2022

JESHI LA POLISI DODOMA LINAWASHIKILIA WATU 129 KWA MAKOSA MBALIMBALI

Na Dotto Kwilasa, DODOMA
JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu 129 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ambao wamekamatwa katika msako mkali pamoja na mali mbalimbali za wizi na watuhumiwa waliokuwa wakitafutwa kwa makosa ya mauaji na wizi wa silaha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Martin Otieno amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari na kueleza kuwa mnamo Mei 4 majira ya saa 3 mkazi wa Kijiji cha Ilangali,Kata ya Manda Tarafa ya Mpwayungu,Wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma Shabani Chilingo (54) ameuawa na mtoto wake aitwaye Shukrani Chilingo (35) chanzo kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.

Amesema chanzo cha mauaji hayo ni mtuhumiwa alimtuhumu baba yake mzazi ambaye ni (Marehemu) kuwa ana mahusiano ya kimapaenzi na mke wake.

Kamanda Otieno ametaja tukio lingine kuwa mnamo tarehe 5 Mwezi May,2022 mtaa wa mailimbili Mnadani jijini hapa Amelia Salamba mwenye Umri wa miezi 10 alikutwa amekufa baada ya kutumbukia kwenye ndoo ya maji yenye ujazo wa Lita 10 iliyokuwa chooni ambapo mtoto huyo alibaki na msichana wa kazi wakati wazazi waeenda kazini.

"Matukio mingine ni Pamoja na wizi wa unyanganyi wa pikipi 17,simu 42 bastola1 Television8, Bangi kgs 36, pombe Moshi Lita 5 ,Mafuta ya Diesel lita75 ,mapanga 4 Kompyuta mpakato 1 na vifaa vya kubadilishia Mfumo Katika simu na kubadilishia IMEI Namba,"amesema.

Pamoja na hayo ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wafike kwenye vituo vya Polisi kutambua mali zao na kwamba operesheni hiyo Bado inaendelea kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia unaimarishwa.

No comments: