Advertisements

Tuesday, March 12, 2024

UZINDUZI WA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR-AN AFRIKA MASHARIKI


Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na waumini wa dini ya kiislam wakati akizindua mashindano ya kuhifadhi Qur-an Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika machi 30 mwaka huu katika viwanja vya Amani Complex hafla iliyofanyika Madinatu Al bahr Mbweni Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ,Katiba , Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Mhe Hemed Suleiman Abdulla kuzindua mashindano ya kuhifadhi Qur -an Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika machi 30 mwaka huu katika viwanja vya Amani Complex hafla iliyofanyika madinatu Al bahr Mbweni Zanzibar.
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakifuatilia uzinduzi wa mashindano ya kuhifadhi Qur -an Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika machi 30 mwaka huu katika viwanja vya Amani Complex hafla iliyofanyika madinatu Al bahr mbweni Zanzibar.
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakifuatilia uzinduzi wa mashindano ya kuhifadhi Qur -an Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika machi 30 mwaka huu katika viwanja vya Amani Complex hafla iliyofanyika madinatu Al bahr mbweni Zanzibar. Picha na Fauzia Mussa --Maelezo Zanzibar.


Na Rahma Khamis Maelezo.
Makamu wa Pili wa Rais Alhaj Hemed Suleiman Abdullah amewataka wazazi na walezi kuwahimiza vijana na jamii kwa ujumla kuzidi kushikamana na Qur-an kwa kuisoma,kuihifadhi na kufuata maamrisho na makatazo yake kwani ndio muongozo kwa wanadamu wote.

Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Madinat-Albahr Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akizindua mashindano ya kuhifadhi Qur-an Afrika Mashariki.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono harakati hizo ambazo dhamira yake ni kuisaidia jamii katika kuendeleza dini ya kiislamu na kuimarisha maadili mema ambayo ni nguzo kwa jamii inayoendele kudumisha amani na umoja uliopo Nchini.

Alhajj Hemed ameongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatambua kazi kubwa zinazofanywa na Ofisi ya Mufti Mkuu na Shirika la Utangazaji Zanzibar katika kujenga jamii yenye maadili mema,hivyo itaendelea kuunga mkono juhudi hizo ili kuona Zanzibar inazalisha vijana wenye kufaata maadili .

"Tunapozungumza Qur-an huwa tunazungumzia maisha ya dunia na na Akhera tunakokwenda hivyo hatuna budi kuisoma na kuihifadhi ili tupate maisha bora zaidi" Alhaj Hemed alisisitiza.

"Ni dhahiri kuwa endapo vijana wetu hatutawawekea misingi imara ya kitabia na kuifahamu dini yao ,watakua rahisi kufuata tamaduni za kigeni ambazo zinakwenda kinyume na mila ,Silla na desturi zetu " alifafanua Makamu wa Pili.

Akitoa maelezo mafupi Katibu Mtendaji Ofisi Mufti Sheikh Khalid Ali Mfaume amefahamisha kuwa mwenye kushika Qur-an Mwenyezi Mungu humuinua hivyo ipo haja kwa waislamu kujitahidi kuisoma na kuhifadhi ili kupata radhi za Allah SW.

Kwa upande Mkurugenzi wa ZBC Ramadhan Bukini amesema kuwa lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuitangaza Qur-an kwani upo umuhimu wa kufanya hivyo kutokana na mwezi wa ramadhani ndipo iliposhushwa Qur-an hiyo.

Mapema alifahamisha kuwa mashindano hayo yatafanyika machi 30 mwezi huu katika Uwanja wa Amani Complex na kuwataka wananchi kujitokeza kuhudhuria kwa wingi ili kupata radhi za Allah.

Mkurugenzi Bukini ameeleza kuwa awali walikua wakifanya mashindano hayo ndani ya Zanzibar kwa njia ya Tartili lakini kwa mwaka huu wameimarisha zaidi kwa kushirikisha nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya Comoro, Burundi ,Uganda na Wenyeji Tanzania.

Mashindano hayo yameandaliwa na Shirika la Utangazaji ZBC kwa kushirikiana na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu “Qur-an ni nguzo ya kutuunganisha”.


No comments: