Advertisements

Monday, April 29, 2024

DK.HUSSEIN ALI MWINYI AMEKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZII WA SAUDI ARABIA NCHINI TANZANIA IKULU ZANZIBAR


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Mhe.Yahya Bin Ahmad Okeish alipofika Ikulu Jijini Zanzibar na ujumbe wake kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Mhe. Yahya Bin Ahmad Okeish, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Mhe. Yahya Bin Ahmad Okeish, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameihakikishia Serikali ya Saudi Arabia ushirikiano mzuri uliopo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mhe. Yahya Ahmad Okeish na ujumbe wake kwa lengo la kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya nchi mbili hizo.

Dk. Mwinyi alisema, SMZ ni mnufaika mkubwa wa mfuko wa Saudia na Quwait kwenye miradi yake ya maeneleo kupitia ushirikiano mzuri uliopo baina ya mataifa hayo.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameishukuru na kuipongeza Serikali ya Saudi Arabia kwa ushirikiano wake na Tanzania hususan kuipatia Zanzibar zawadi mbalimbali inazozituma kwa watu wa Zanzibar ikiwemo tende wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Katika salamu zake kwa Tanzania, Balozi Okeish amepongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na taifa hili kwa kutimiza miaka 60 ya Muungano wake baina ya Tanganyika na Zanzibar sambamba na kuuombea mafanikio zaidi muungano huo.

Pia, Balozi Okeish alisifu ushirikiano wa diplomasia uliopo baina ya Saudi Arabia na Tanzania ikiwemo Zanzibar pamoja na kusifu tamaduni za pande mbili hizo.



IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.

No comments: