Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akiwa pamoja na Katibu Mkuu Balozi Aisha Amour, na viongozi mbalimbali wakikagua miundombinu ya barabara ya Mwaikibaki (Morocco-Africana), ambayo inatarajiwa kufanyiwa upanuzi kuwa njia nne, Mkoani Dar es salaam.
Mafundi wakiendelea na kazi ya urejeshaiji qa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha changarawe katika barabara ya Bunju B - Mpiji Magoe, Mkoani Dar es Salaam.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Dar es salaam, Mhandisi John Mkumbo, akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwaikibaki (Morocco-Africana), yenye urefu wa kilomita 11.7 ambayo inatarajiwa kufanyiwa upanuzi na kuwa ya njia nne, Mkoani Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akizungumza na kusikiliza wananchi wakazi wa Mikocheni, wakati akikagua barabara ya Mwaikibaki (Morocco-Africana) ambayo inaenda kufanyiwa upanuzi na kuwa njia nne Mkoani Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment