Advertisements

Saturday, May 4, 2024

TANZIA : ALIYEWAHI KUWA WAZIRI WA FEDHA MUSTAPHA MKULO AFARIKI DUNIA


Mustafa Mkulo enzi za uhai wake

ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi, Mhe. Mustapha Haidi Mkulo, amefariki dunia Mei 4, 2024 akiwa na umri wa miaka 78.

Taarifa iliyopatikana jijini Dar Es Salaam imesema, marehemu Mkulo amefariki akiwa anapatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbuili, jijini Dar Es Salaam.

Marehemu Mkulo ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Kilosa mkoani Mororogoro, aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango na Rais wa Awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete mwaka 2005 hadi 2012.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na mke wa marehemu, Bi. Julie Mkulo, leo Mei 4, 2024 limesema mwili wa marehemu Mkulo utaswaliwa katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam, Mei 4, 2024, na mazishi yatafanyika wilayani Kilosa Mei 5, 2024.

No comments: