Monday, June 24, 2024

MWENGE WA UHURU NI TUNU YA TAIFA,UHESHIMIWE,ULINDWE NA UPENDWE


Katibu wa siasa itikadi na uenezi wa CCM mkoa wa Iringa Joseph Ryata akiwa ameshika Mwenge wa uhuru ulipowasili mkoani Iringa.
katibu wa siasa itikadi na uenezi wa CCM mkoa wa Iringa Joseph Ryata akisalimiana na mmoja ya wakimbiza Mwenge wa uhuru kitaifa.

Na Fredy Mgunda, Iringa.
Wananchi wameombwa kuendelea kuuheshimu,kuulinda na kuupenda mwenge wa uhuru kitaifa ambao umekuwa ukimulika miradi mingi ya kimaendeleo hapa nchini Tanzania.

Akizungumza Katibu wa siasa itikadi na uenezi wa CCM mkoa wa Iringa Joseph Ryata alisema kuwa kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakiubeza mwenge wa uhuru kuwa hauna tija jambo ambalo sio kweli.

Ryata alisema kuwa Mwenge wa uhuru unatija kubwa kwa kuwakumbusha viongozi wa serikali namna bora ya uwajibikaji na uzalendo hivyo wananchi wanatakiwa kuwa wazalendo na Mwenge wa uhuru.

Alisema kuwa Mwenge wa uhuru kitaifa huwa unakuja na kauli mbiu mbalimbali ambazo huamasisha maendeleo ya wananchi na serikali kwa ujumla ndio maana ujumbe wake huwa unabeba taswira ya maendeleo kwa mwaka huo.

Mwenge wa uhuru unapita kwe miradi ya sekta mbalimbali elimu,afya,miradi ya kiuchumi, Miundombinu na miradi ya kijasiliamali na miradi ya kijamii

Katika mkoa wa Iringa Mwenge utakimbizwa wilaya zote 3 wilaya ya Mufindi ,kilolo,na wilaya ya Iringa na jumla ya Miradi 50 itapitiwa na kukaguliwa

No comments: