Tuesday, July 30, 2024

KILIMANIHEWA KUPEWA ELIMU NAMNA YA UTUNZAJI NA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA


Baadhi ya wajasiriamali na makundi maalum wa Kilimanihewa mkoani Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa masuala ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi za Fedha baada ya kupatiwa mafunzo ya elimu ya fedha mkoani humo.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii, Bw. Ambros Ngwadakulima akizungumza na Timu ya wataalamu ya Wizara ya Fedha na wataalamu kutoka Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) walipofika Ofisini kwake kabla ya kuanza kutoa elimu ya fedha.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii, Bw. Ambros Ngwadakulima, (katikati) Afisa Mkuu Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha - Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro (wa kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalamu wa kutoa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha, walipofika Ofisini kwake kabla ya kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na wananchi wa Mtwara.
Afisa Mkuu Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha - Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro akitoa elimu ya Fedha kwa wanavikundi, wajasiriamali na makundi maalum katika ukumbi wa Kilimanihewa mkoani Mtwara.
Mratibu/Msajili Huduma Ndogo za Fedha Bi. Angela Aore, akizungumza na wananchi wa Kilimanihewa wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha inatolewa na watalaamu wa Wizara ya Fedha.
Afisa Mkuu wa Bima wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Bi. Gladness Lema, akitoa elimu ya Fedha kwa wanavikundi, wajasiriamali na makundi maalum katika ukumbi wa Kilimanihewa mkoani Mtwara.
Baadhi ya wajasiriamali na makundi maalum wa Kilimanihewa mkoani Mtwara wakipatiwa mafunzo ya elimu ya fedha na Wizara ya Fedha wakishirikiana na Taasisi za Fedha mkoani Mtwara.
Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha - Wizara ya Fedha, Bw. Jackson Mushumba akitoa elimu ya Fedha kwa wanavikundi, wajasiriamali na makundi maalum katika ukumbi wa Kilimanihewa mkoani Mtwara.
Afisa Sheria Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonza, akitoa elimu ya fedha kwa wanavikundi, wajasiriamali na makundi maalum katika ukumbi wa Kilimanihewa mkoani Mtwara.
Baadhi ya wajasiriamali na makundi maalum wa Kilimanihewa mkoani Mtwara wakipatiwa mafunzo ya elimu ya fedha na Wizara ya Fedha wakishirikiana na Taasisi za Fedha mkoani Mtwara.
Baadhi ya wajasiriamali na makundi maalum wa Kilimanihewa mkoani Mtwara wakipatiwa mafunzo ya elimu ya fedha na Wizara ya Fedha wakishirikiana na Taasisi za Fedha mkoani Mtwara.

Baadhi ya wajasiriamali na makundi maalum wa Kilimanihewa mkoani Mtwara wakipatiwa mafunzo ya elimu ya fedha na Wizara ya Fedha wakishirikiana na Taasisi za Fedha mkoani Mtwara.

Baadhi ya wajasiriamali na makundi maalum wa Kilimanihewa mkoani Mtwara wakipatiwa mafunzo ya elimu ya fedha na Wizara ya Fedha wakishirikiana na Taasisi za Fedha mkoani Mtwara.

Na Chedaiwe Msuya, WF, Mtwara
Wafanyabiashara wametakiwa kujenga tabia ya kuweka akiba katika biashara zao ili kuhakikisha wanakuwa na maendeleo endelevu.

Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonza, alitoa wito huo alipokuwa akitoa elimu ya utunzaji na matumizi sahihi ya fedha katika ziara ya utoaji elimu ya fedha kwa umma wilayani Masasi mkoani Mtwara.

Akitoa elimu hiyo ya fedha, Bw. Myonza aliwasisitiza wafanyabiashara kujiepusha na matumizi ya pesa zote wanazozipata na badala yake waweke akiba ya sehemu ya mapato yao.

"Ndugu wafanyabiashara, tujenge tabia ya kujiwekea akiba katika biashara au katika mapato tunayopata katika utafutaji wetu." Alisema Bw. Myoka.

Alitoa mfano wa mfanyabiashara anayepata shilingi laki moja, anashauriwa kutumia shilingi elfu sitini na kuweka shilingi elfu arobaini kama akiba kwani itamsaidia baadaye.

Aliwaasa wafanyabiashara kuacha tabia ya kutumia pesa zote kwa kisingizio cha kujipongeza, kwani kufanya hivyo kunawarudisha nyuma kimaendeleo.

Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii, Bw. Ambros Ngwadakulima, eneo la Kilimanihewa amewaeleza wananchi wa Mkoa wa Mtwara kutoa ushirikiano kwa wataalamu na kuwaasa kujiunga katika vikundi vilivyokuwa rasmi, pia alisistiza wale wote wanaotoa huduma za fedha kinyume na utaratibu wa kisheria kuchukuliwa hatua.

Bi. Maisha Raimondi, mfanyabiashara kutoka kijiji cha Makanga, alitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwaruhusu wataalam kutoka Wizara ya Fedha kuzunguka mikoani kutoa elimu ya utunzaji na matumizi sahihi ya pesa.

Alisema kuwa elimu hiyo itawasaidia sana wafanyabiashara kuendesha biashara zao kwa mafanikio na kuhakikisha kunakuwa na maendeleo endelevu.

Katibu wa vikao, Bw. Ismail Rashidi, kutoka Kata ya Kilimanihewa, ameipongeza Serikali kwa kutambua kuwa mkoa wa Mtwara kuwa miongoni mwa wanufaika wa elimu hiyo.

Aliendelea kusisitiza umuhimu wa wananchi wa Kilimanihewa kuacha tabia ya matumizi mabaya ya fedha na kuwekeza katika taasisi zilizosajiliwa ili kuhakikisha usalama wa fedha zao.

Afisa Mkuu wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Bi. Gladness Lema, aliwahimiza wananchi kuwa na bima itakayoweza kuwasaidia katika maafa mbalimbali yatakayojitokeza katika shughuli za kilimo na kuweza kupata fidia kutokana na bima watakayoikata.

Wataalam hao walisema kuwa Mtwara ni mkoa wa tisa tangu wameanza kutoa elimu hiyo, wakitimiza maagizo ya Mhen. Rais kupitia Wizara ya Fedha kuzunguka nchi nzima kutoa elimu ya fedha.

No comments: