ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 28, 2024

DKT. NATU AKUTANA NA UJUMBE WA IMF, WB NA COMSEC


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati wa kikao na Ujumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola (COMSEC), kwa ajili ya kufunga zoezi la kutathmini ubora wa Takwimu za Madeni ya Sekta ya Umma (PSDS)), kilichofanyika Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiongoza mkutano na Ujumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola (COMSEC), kwa ajili ya kufunga zoezi la kutathmini ubora wa Takwimu za Madeni ya Sekta ya Umma (PSDS), kilichofanyika Jijini Dodoma.

Na. Asia Singano, WF, Dodoma
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El maamry Mwamba, amekutana na Ujumbe wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola (COMSEC), kwa ajili ya kufunga zoezi la kutathmini ubora wa Takwimu za Madeni ya Sekta ya Umma (PSDS), nchini Tanzania.

Zoezi hilo lilifanywa kuanzia tarehe 23 hadi 27 Septemba 2024 ambapo ujumbe huo ulikutana na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wizara mbalimbali na Taasisi za Serikali ambapo pamoja na mambo mengine tathmini hiyo ililenga kuangalia na kubaini ubora na mapungufu yaliyopo katika ukusanyaji, uchakataji na usambazaji wa takwimu hizo.

No comments: