ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 9, 2024

NBAA YAWANOA WAKUFUNZI KUHUSU MTAALA MPYA

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania ( NBAA) CPA Pius A. Maneno akifungua mafunzo kwa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi iliyofanyika katika Ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Elimu ya Taaluma na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo (kulia) akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo na namna yatakavyosaidia kuongeza ufaulu kwa watahiniwa wa Bodi.
Baadhi ya wakufunzi wa vituo vya kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi  pamoja na wafanyakazi wa NBAA wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania ( NBAA) CPA Pius A. Maneno wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mkufunzi CPA Rashid Mganwa akitoa maelezo kuhusu mabadiliko ya mtaala kwenye masomo ya A3, A4, A6, B1, B2, B3, B4, C3 na C4 nk. kwa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi.
Mkufunzi CPA Edson Leoncy  akiwasilisha mada kwa wakufunzi wa vituo vya kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi.

WAKATI serikali ikiendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya fedha kwenye Taasisi ambazo inazisimamia ili kuweza kupatiwa hati safi baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kimahesabu, Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA)  imewataka wakufunzi wanaofundisha masomo ya Uhasibu kuachana na njia za zamani za kufundishia na kujikita kwenye njia za kisasa zinazoendana na ukuaji wa teknolojia

Akuzungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Wakufunzi wanaofundisha watahiniwa wa Mitihani ya Bodi,  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo CPA Pius A. Maneno amesema wataalamu wa mambo husema biashara asubuhi jioni mahesabu, hii ni kauli ambayo inatumika sana katika jamii ikilenga kuweka utayari kwa mtu au watu kutekeleza mipango ya maendeleo mapema kabla ya kufika malengo husika hapo baadae.

Amesema Bodi itafanya mapitio ya matokeo ya awali ya mitihani yaliyopitishwa na Kamati ya Bodi ya Elimu ya taaluma na Mafunzo na baada ya hapo mtahiniwa ataruhusiwa kukata rufaa ya matokeo yake baada ya kupitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya NBAA ambapo taratibu huu utaanza kwa mitihani iliyofanyika mwezi wa nane mwaka 2024.


No comments: