ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 10, 2024

TAWLA YAWAPIGA MSASA WANAHABARI


Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya siku mbili kwa wanahabari yenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye uandishi/utoaji habari zenye kuchechemua marekebisho ya sheria na upitishwaji wa sera zinazolinda afya ya jamii
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Wakili Tike Mwambipile akizungumza kuhusu historia ya kuanzishwa kwa chama hicho wakati wa mafunzo wanahabari yenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye uandishi/utoaji habari zenye kuchechemua marekebisho ya sheria na upitishwaji wa sera zinazolinda afya ya jamii.
Meneja Mwandamizi wa Mawasiliano, Afrika kutoka Global Health Advocacy Incubator (GHAI), Bobi Odiko akizungumza kuhusu lengo lao la kusaidia nchi na mashirika ya afya kuunda na kutekeleza sera zinazosaidia kuboresha afya ya umma kwa kutumia mbinu za kitaalamu na uhusiano mzuri na wadau muhimu ili kuhakikisha kwamba sera zinazotekelezwa zina athari chanya katika maisha ya watu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) pamoja na waandishi wa habari wakifuatlia mada wakati wa mafunzo wanahabari yenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye uandishi/utoaji habari zenye kuchechemua marekebisho ya sheria na upitishwaji wa sera zinazolinda afya ya jamii.

Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kinaendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini ikiwa na lengo  la kuwajengea uwezo kwenye uandishi/ utoaji habari zenye kuchechemua marekebisho ya sheria na upitishwaji wa sera zinazolinda afya ya jamii inayofanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema waandishi wa habari wanabidi kuzingatia maadili na ubora katika kazi za uandishi ikiwemo na uzingatiaji wa sheria zilizowekwa.

"MCT itaendelea kushirikiana na wadau kama TAWLA ili kuhakikisha habari zinazohusiana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza zinafika kwa umma kwa lengo la kuhamasisha mapambano dhidi ya magonjwa hayo." alisema Sungura

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Wakili Tike Mwambipile amesema ukosefu wa mazoezi ni mojawapo ya sababu kubwa zinazochangia magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile magonjwa ya moyo na kisukari. 

Pia ametoa wito kwa jamii kufanya mazoezi na kutumia vyakula bora kwa kuwa gharama kubwa zinatumika katika kutibu magonjwa yasiyoambukizwa









No comments: