Na Mwandishi Jeshi la Polisi Arusha.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linamshikilia Jaina Mchomvu kwa tukio la mauaji ya mtoto aitwaye Mariam Juma mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa kwa Mrombo katika Halmashauri ya jiji la Arusha aliyekutwa ameauwa huku mwili wake ukiwa na majeraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya shingoni na maeneo mbalimbali ya mwili wake kisha mwili wake ukifichwa chini ya uvungu wa kitanda kwenye nyumba ya jirani yao.
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema awali mtoto huyu alikuwa ametumwa dukani toka asubuhi lakini hakurejea na ilipofika mchana wazazi wake walianza kumtafuta maeneo mbalimbali baada ya kuingiwa na wasiwasi.
SACP Masejo amesema hadi sasa tunawashikilia watu watatu akiwepo Jaina Mchomvu Mama mwenye nyumba ambaye amekamatwa na askari Polisi huko Mabogini Moshi, Mkoani Kilimanjaro alikokimbilia kujificha baada ya tukio hili kubaainika, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
SACP Masejo amesema kuwa Baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa Jaina Mchomvu alihojiwa na kukiri kutenda tukio hilo la mauaji ya mtoto huyo.
Amefafanua kuwa Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za kiuchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Jeshi la Polisi Mkoani humo limewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu huku Jeshi hilo likiwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kuhusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment