Tuesday, October 8, 2024

TOTALENERGIES KWA KUSHIRIKIANA NA NAFASI ART SPACE WATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KATIKA SHULE YA MSINGI YA UZURI


Meneja Mawasiliano wa TotalEnergies Marketing Tanzania ltd Anita Bulindi akizungumza na wanafunzi wa Shule ya msingi ya Uzuri wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo wakishirikiana na Taasisi ya Nafasi Art Space wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Mwezeshajiwa mradi kutoka Nafasi Art Space Michael James akizungumza namna walivyowawezesha wanafunzi 20 kuweza kuchora michoro mbalimbali ya usalama Barabarani na kuiwasilisha kwa wanafunzi wenzao wa Shule ya msingi ya Uzuri.
Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi ya Uzuri Rehema Athanus Mapunda akiwakaribisha na kuzungumza masuala mbalimbali kuhusu shule hiyo kwa  baadhi ya wafanyakazi wa TotalEnergies Marketing Tanzania ltd waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu usalama barabarani wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Mwanafunzi wa darasa la Sita na balozi Balozi wa Usalama barabarani katika Shule ya msingi ya Uzuri Jamal Ally akitoa elimu kuhusu alama za usalama barabarani kwa wanafunzi wenzake wakati wa mafunzo hayo 
 Mwanafunzi wa darasa la Sita na balozi Balozi wa Usalama barabarani katika Shule ya msingi ya Uzuri Pheb William akitoa mapendekezo kuhusu mambo ya kufanywa katika barabara zilizopo pembezoni mwa shule hiyo wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya mafuta ya TotalEnergies Tanzania, walimu na wanafunzi wa Shule ya msingi ya Uzuri wakifuatlia elimu ya usalama barabarani iliyokuwa inatolewa na mabalozi wa usalama barabarani kutoka shuleni hapo.
Picha za pamoja 

Ikiwa kwenye wiki ya huduma kwa Wateja Kampuni ya mafuta ya TotalEnergies kwa kushurikiana na Taasisi ya Nafasi Art Space wametoa elimu ya usalama barabarani katika shule ya msingi ya Uzuri iliyopo katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo meneja Mawasiliano wa TotalEnergies Marketing Tanzania ltd Anita Bulindi amesema kwa miezi minne wameweza kutoa elimu ya usalama Barabarani katika shule ya  msingi ya Uzuri ambapo wameweza kupata mabalozi 20 ambao leo wameweza kutoa elimu kwa wanafunzi wenzao ili kufahamu taratibu mbalimbali za usalama barabarani.

Amesema Shule hiyo imewahamasha kuendelea kutoa elimu kwa wanafunzi katika shule mbalimbali kwani wameona kuna haja hiyo kwasababu ya kuwezesha wanafunzi kuzifahamu sheria za usalama barabarabini ili kulinda Maisha ya wanafunzi hao wanapotumia barabara.

Naye mkuu wa shule Mwalimu mkuu wa Shule ya msingi ya Uzuri Rehema Athanus Mapunda ameishukuru Kampuni ya mafuta ya TotalEnergies kwa kuweza kuichagua shule hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule hiyo kwani kufanya hivyo wameweza kuokoa Maisha ya wanafunzi hao wanaotumia barabara wakati wa kuja shule na kurudi nyumbani.

No comments: