Thursday, October 3, 2024

TOTALENERGIES YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUZINDUA KITUO CHA MAFUTA


Mkurugenzi wa Mtandao wa Vituo vya mafuta TotalEnergies Abdulrahim Siddique pamoja na Mkurugenzi wa Kituo cha Mafuta cha TotalEnergies cha Makanya Thabit Amer wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha mafuta cha TotalEnergies cha Makanya ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja
Mkurugenzi wa Mtandao wa Vituo vya mafuta TotalEnergies Abdul Rahim Siddique akizungumza kuhusu namna Kampuni ya TotalEnergies ilivyijipanga kutoa huduma katika kituo hicho wakati wa uzinduzi wa Kituo cha mafuta cha TotalEnergies kilichopo Makanya, Magomeni jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mafuta cha TotalEnergies cha Makanya Thabit Amer akizungumza kuhusu uwekezaji uliofanywa pamoja na nmna watakavyotoa huduma katika kituo hicho wakati wa uzinduzi wa Kituo cha mafuta cha TotalEnergies kilichopo Makanya, Magomeni jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.
Meneja Masoko wa TotalEnergies, Caroline Kakwezi akizungumza kuhusu Kampuni ya TotalEnergies inavyoendelea kufungua njia kwa makampuni mbalimbali kuweza kufungu vituo vya mafuta kwa chapa ya TotalEnergies ili kuweza kutoa huduma iliyobora kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa Kituo cha mafuta cha TotalEnergies kilichopo Makanya, Magomeni jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya TotalEnergies pamoja na wadau mbalimbali wa kampuni hiyo wakifuatilia uzinduzi wa Kituo cha mafuta cha TotalEnergies kilichopo Makanya, Magomeni jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja

KAMPUNI ya Mafuta nchini TotalEnergies imeendelea kuwafikia watanzania wenye malengo ya kumiliki vituo vya mafuta kwa kuzindua kituo kipya cha mafuta cha TotalEnergies cha Makanya kilichopo jijini Dar es Salaam kinachomilikiwa na Kampuni ya Arasco Energies huku ikielezwa kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa watanzania pamoja na kushirikiana nao katika uwekezaji wa sekta hiyo ili kujenga uchumi wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa wateja.

Akizungumza mara baada ya kuzindua kituo hicho Mkurugenzi wa Mtandao wa Vituo vya mafuta TotalEnergies Abdulrahim Siddique amesema mahusiano hayo ni hatua kubwa katika kuendeleza soko la mafuta nchini na ni fursa kwa watanzania wenye maeneo na ndoto ya kumiliki vituo vya mafuta.

Amesema TotalEnergies inathamini mchango na ushirikiano kutoka kwa wateja wao kupitia huduma na bidhaa wanazotoa, wanawakaribisha wawekezaji wengi zaidi na watapokea maoni ya watanzania ili kuendelea kuboresha huduma wanazozitoa.

Kwa upande wake mmiliki na mwendeshaji wa kituo hicho Thabit Amer amesema amekuwa na ndoto ya kufanya kazi na kampuni ya TotalEnergies kutokana na ubora wa huduma wanazozitoa na ubia huo wa kufanikisha uzinduzi wa kituo hicho utanufaisha pia wakazi wa maeneo hayo kwa huduma za mafuta na vilainishi.


No comments: