Tuesday, November 26, 2024

CCM YAJIVUNIA MAENDELELEO YALIYOFANYWA NA RAIS SAMIA


 *CPA Makalla asema wana matumaini makubwa ushindi Serikali za Mitaa *Asisitiza CCM haitaji mbele wala kubebwa, apiga kijembe Chadema

KATIBU wa Halmashauri Kuu NEC ya Chama Cha Mapinduzi CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amoss Makalla, Akizungumza katika mwendelezo wa kampeni zake za uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu katika Jimbo la Ukonga leo tarehe 24, NOV 2024 ( PICHA NA CCM)

Na Mwandishi Wetu.
KATIBU wa Halmashauri Kuu NEC ya Chama Cha Mapinduzi CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amoss Makalla amesema ushindi wa Chama hicho unatokana na imani ya wananchi inayotokana na kazi nzuri ambazo zimefanywa na Rais DK.Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo nchini kote.

CPA Makalla amesema hayo jana jijini Dar es Salaam akiwa katika mwendelezo wa kampeni zake za uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu na kueleza kwamba Rais Samia amefanya maendeleo makubwa ya yanayoonekana kwa uwazi.

Akiwa katika Jimbo la Ukonga CPA Makalla ameeleza hatua kwa hatua kuhusu maendeleo ambayo Rais Samia ameyafanya nchini na mazuri hayo ndio yanayowapa matumaini kwa wagombea wa CCM kushinda kwa kishindo.

“CCM inabebwa na kazi nzuri zinazofanywa na wabunge na madiwani wake, hivyo tunaimani CCM inauzwa na kazi nzuri iliyofanywa na waheshimiwa wabunge, madiwani na Mheshimiwa Rais, kwani kazi zake zinaonekana,” amesisitiza.

Ameongeza kuwa CCM wanatembea kifua mbele kwa ajili ya kiongozi wao ambaye ni mwenyekiti kitaifa Rais Samia Suluhu Hassan na 4R zake na fedha anazozitoa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

CPA Makalla amefafanua kuwa yote ambayo wapinzani walikuwa wakiyapigia kelele Rais Samia ameyafanyia kazi,hivyo wapinzani katika kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu wamekosa hoja za kuwaambia wananchi na tayari wameshakubali kushindwa katika uchaguzi huo.

"Wapinzani wamekosa haja za kueleza katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwasababu Rais DK.Samia Suluhu Hassan amewafilisi. Kimsingi Rais Samia amegusa yote ambayo wapinzani walikuwa wanayalalamikia.Leo hawana cha kuwaambia Watanzania."

Amesema chini ya uongozi wa Rais Samia kampeni wanafanya kampeni zake kwa kutuata R4 ,hivyo kampeni zao zitakuwa za kistaarabu na hawatamkejeli mtu kwani kuna maendeleo mengi yakuelezea ambayo Rais ameyafanya katika maeneo mbalimbali nchini.

"Wana CCM wanatembea kifua mbele kwasababu ya mambo makubwa ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amefanya nchini kwetu,"amesema na kusisitiza kwa maendeleo ambayo Rais ameyafanya kuna idadi kubwa ya wagombea wa vyama vya upinzani wako katika orodha ya wanaotaka kurudi CCM"

"Kila mahali Rais Samia amepeleka fedha , ametekeleza miradi na ndio maana leo katika mkutano huu tunaye kiongozi wa kitaifa waTLP ameamua kuja kuungana na Wana CCM kuomba wananchi wachague wagombea wa CCM."

Pamoja na hayo amesema wakati viongozi wa CCM wakiwatumikia Watanzania katika kuleta maendeleo vyama vya upinzani hasa CHADEMA wao walikuwa wakihamasisha maandamano na kimsingi maandamano hayo yamewasaidia zaidi kupata fedha lakini wanachama wao wakifanyishw mazoezi yasiyo na faida kwao wala kwa Taifa.

Hivyo amesema kuna kila sababu ya kuwaomba wananchi kuchagua wagombea wa Chama hicho na kusisitiza Chama hicho hakihitaji mbeleko kwasababu kwa mambo yaliyofanywa na Rais Samia, Wabunge na Madiwani wanauhakika wa kushinda.

"Tutashinda kwasababu yaliyofanywa na Rais Samia yanatufanya tuwe na imani na ushindi wa kishindo.Kazi zetu ndizo zinatupa ushindi,"amesema na kusisitiza kwa sasa wabunge na madiwani wengi ni wa CCM hivyo hata alipatikana mgombea wa upinzani anakwenda kufanya kazi na nani.

Akielezea zaidi katika mikutano ya kampeni anayoendelea kuifanya CPA Makalla amemsikia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akisema kuwa wagombea wao ni waaminifu lakini ukweli Chama hicho hawana uaminifu wowote huku akikumbusha Wabunge 19 wa Chama hicho waliofukuzwa na kuwaita COVID-19 .

"CHADEMA hawaamini kabisa na mnakumbuka waliwafukuza Wabunge wao 19 na wakaanza kuwaita majna mabaya,lakini Wabunge hao walikwenda mahakamani wakishinda kesi na sasa wanachukua ruzuku.

"Sasa la kujiuliza kama waliwafukuza Wabunge wao mnaujakika gani wakipata wagombea katika Serikali za Mitaa hawatawafukuza? Ndio maana nawaomba Watanzania msipoteze muda na wapinzani hawaamini lakini hata Ilani hawa a zaidi kuwa wanabuni na kufikiria kutoka katika vichwa vyao,"amesema CPA Makalla.

Kuhusu kampeni za uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji zinatarajia kumalizika Novemba 26 mwaka huu lakini CCM imejiridhisha kuwa itashinda uchaguzi huo kwani wagombea wao wanazo sifa zote na wamechujwa na vikao vya Chama.

Amewakumbusha umuhimu wa Wana CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura Novemba 27 mwaka huu ili kuhakikisha wagombea wa Chama hicho wanashinda kwa kishindo na kufafanua katika uchaguzi huo kutakuwa na kura ya ndio na hapana,hivyo ili kuwa na uhakika wa kura .

"Twendeni tukapige kura ili tushinde kwa kishindo,tushinde ushindi wa heshima.Asitokee mtu wa kuwadanganya kuwa katika Mitaa ambayo wapinzani hawajasimamisha wagombea usiende kupiga kura.Wote tukapige kura ya ndio kuhakikisha ushindi unakuwa wa kishindo."

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake