Tuesday, November 26, 2024

JESHI LA POLISI KAGERA LAPOKEA MAGARI MATANO KUIMARISHA ULINZI


Na Mariam Kagenda _Kagera

Jeshi la polisi mkoani Kagera limepokea magari matano kwa ajili ya kuimairisha ulinzi na usalama katika kipindi hiki Cha kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu siku ya Jumatano.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Kagera Brasius Chatanda amesema kuwa wanachi wasiwe na wasiwasi katika kipindi hiki badala yake wajitokeze kwa wingi kusikiliza sera za Vyama vyote kwenye kampeini pamoja na kujua ni mgombea Gani watampa dhamana ya kuwaongoza.

Amesema kuwa siku ya kupiga kura Novemba 27 wanachi wasiwe na wasiwasi kwa sababu Jeshi hilo limejipanga vizuri kwani amani na utulivu ndio kipaumbele Cha kwanza .
"Tulikuwa na changamoto ya vitendea kazi , serikali imeliona Hilo na Jeshi la polisi tumepata vitendea kazi ,hivi karibuni pia tulipokea magari mawili ,natoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanasikiliza kampeini kikamilifu ,na kuchagua kwa amani Jeshi la polisi tuko tayari kulinda amani katika mkoa wa Kagera"

Ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanawachagua viongozi Bora ambao watakuwa nao bega kwa bega katika maswala ya kuwaletea maendeleo.




No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake