Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Novemba 20, 2024, amehudhuria katika Mkutano wa Dunia kuhusu Utalii, Uchumi wa Buluu, Bahari na Mazingira.
Mkutano huo wa Siku Mbili, ambao umeanza leo, unafanyika katika Hoteli ya Cabo de Gata, Jijini Almeria, Nchini Hispania.
Wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo, Viongozi mbali mbali, wakiwemo Wakuu wa Taasisi ya Kimataifa ya 'the Sun and Blue Congress', wameshukuru Hatua ya Mheshimiwa Othman na Ujumbe wake, kuhudhuria Mkutano huo wa Kimataifa.
Akiwasilisha Mada ya Fursa za Utalii Zilizojaa katika Maeneo mbali mbali ya Uchumi wa Buluu, Bingwa na Mtaalamu wa Masuala ya Mazingira Ulimwenguni, Profesa Gunter Pauli, ameishukuru Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutokana na Fursa ilizompatia yeye na Taasisi nyengine, tangu Mwaka 1993, alipofika kwaajili ya Kusaidia Mbinu za Uzalishaji wa Zao la Mwani, na pia Mapambano dhidi ya Uvuvi Haramu wa Baruti.
Amefahamisha kuwa hadi alipoikamilisha Kazi hiyo, tayari alkwishafanikisha kupatikana kwa Ajira takriban Elfu Ishirini na Tatu (23) kupitia Utalii, Mwani, na Uchumi wa Buluu.
Hivyo, ameishauri Zanzibar kutumia Uzuri wake wa Asili, pamoja na Mazingira yake yenye kuvutia, ili kuimarisha Sekta ya Utalii, na pia kusaidia katika kujiimarisha kiuchumi.
Mtaalamu huyo na Mtunzi Mashuhuri wa Vitabu, katika Fani za Mazingira, Uchumi wa Buluu, Utalii na Teknolojia, ameahidi kuisaidia Zanzibar, kupata Fursa nyingi za Maendeleo, kupitia Taasisi za Kimataifa ambazo anashirikiana nazo.
Baada ya Ufunguzi wa Mkutano huo, Mheshimiwa Othman amekuwa na Mikutano Maalum ya Kujadili, namna ambavyo Zanzibar inaweza kujikwamua kiuchumi, kupitia fursa mbali mbali, ziliopo Nchini.
Katika Vikao Muhimu vya Mkutano huo, Mheshimiwa Othman wamembatana na Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa ambaye pia anahudumu Nchini Hispania, Balozi Ally Jabir Mwadin, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendeshaji na Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) Ndugu Sheha Mjaja Juma.
Mheshimiwa Othman yupo ziarani nchini Hispania akiambatana pia na Mke wake Mama Zanab Kombo Shaib.
Kitengo cha Habari, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Novemba 20, 2024.
No comments:
Post a Comment