ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 10, 2025

BARAZA LA WAFANYAKAZI PSPTB LAFUNGULIWA


Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi akizungumza wakati wa kufungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB likilokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo lililofanyika mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa TUGHE PSPTB, Shilla Mwandu akizungumza kuhusu namna wafanyakazi wanabidi kujitadhmini pale wanapokuwa wanafanya kazi za Serikali wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB lililofanyika mkoani Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa PSPTB wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa kwenye kikao kazi kilichokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSPTB pamoja na wageni waalikwa wakati wa wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB likilokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo.

BODI ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imefanya kikao cha Baraza la wafanyakazi leo ili kujadili mafanikio, changamoto na njia za kuweza kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa uundaji wa bajeti mwaka unaokuja wa 2025/2026.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu Ununuzi na Ugavi Godfred Mbanyi amesema baraza ni chombo kinachoundwa na sheria ya Mahusiano kazini kwa ajili na kuweka mazingira mazuri mahali pakazi ambapo chombo hiki kinawiwa kwa mkataba baina na Menejimenti pamoja na chama cha wafanyakazi sehemu ya kazi.

Pia amasema Baraza la leo limefanyika ili kutathmini utendaji kazi wa bajeti ya mwaka ujao wa fedha wa 2025/2026, kisheria na kiutaratibu bajeti yoyote kabla haijahidhinishwa lazima ipitishwe na Balaza la Wafanyakazi sehemu ya kazi.

Mbanyi amesema Bajeti ya mwaka 2024/2025 inatilikamilika Juni 30, 2025 hivyo ni wajibu wa menejimenti kuja kueleza balaza nini mafanikio, changamoto na njia za kuweza kutatua changamoto zilizojitokeza ili inapoundwa bajeti mpya ya mwaka mpya wa Serikali kunakuwa na vipaumbele vyake.

“Umuhimu wa Mabaraza ya kazi kwanza yanaleta ushirikishwaji wa wafanyakazi sehemu ya kazi hivyo wafanyakazi wanakuwa ni sehemu ya maamuzi katika Taasisi, kwaiyo Taasisi sio kwamba inakuwa inaongozwa na Menejimenti lakini inakuwa na chombo ambacho kinawakilisha wafanyakazi wote katika taasisi mbalimbali.” Alisema Mbanyi

No comments: