ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 3, 2025

RAIS WA ZANZIBAR DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA MWANAZUONI DR. ZAKIR NAIK IKULU ZANZIBAR


Raus wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mwazuoni Dk.Zakir Naik, (kulia kwa Rais) alipofika Ikulu na Ujumbe wake kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wq Zanzibar Mhe. Sheikh Saleh Omar Kabi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema dhana ya Utalii wa Maadili inaendelea kukua zaidi kufuatia Ujio wa Viongozi mbalimbali wa Kiimani nchini.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Mwanazuoni Dk, Zakir Naik wa Taasisi ya Putrajaya ya Malaysia na Ujumbe wake waliofika Ikulu kuonana naye.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar Imekuwa na fursa kubwa ya kuendeleza Utalii na ajira kwa Vijana kufuatia utekelezaji wa dhana hiyo ya utalii wa Maadili iliokubalika na jamii

Rais Dk.Mwinyi amemsisitiza Mwanazuoni huyo kuyatembelea Maeneo zaidi ya Kihistoria yaliopo nchini na kuwa Balozi wa Kuitangaza Zanzibar Kimataifa.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amemshauri Dk.Zakir kufikiria Kuitembelea Zanzibar Kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa lengo la kufanya Mihadhara kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu.

Naye Dk.Zakir Naik amesifu Maendeleo yanayofikiwa nchini pamoja na muendelezo Mzuri wa harakati za Dini ya Kiislamu hapa nchini na kuahidi ushirikiano.

No comments: