Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Awali Juma Fimbo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAA Abdul Mombokaleo wakikabidhi mkono wa Sikukuu ya Eid kwa kituo cha kulelea watoto cha Zili wakati wa futari iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo.
Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) imewakutanisha pamoja Wadau , Wafanyakazi wake na Watoto yatima katika hafla ya Iftar iliyofanyika katika Jengo la 3 la abiria Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Katika Iftar hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TAA Bw, Abdul Mombokaleo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania Awali Juma Fimbo wamekabidhi zawadi ya mkono wa Eid kwa watoto yatima kutoka kituo cha kulelea watoto cha Zili kinachopatikana Kata ya Airport waliojumuika pamoja na Wadau wengine katika hafla hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya kurudisha kwa jamii kwa wananchi wa maeneo yanayozunguka viwanja vya ndege ili kujenga mahusiano mema.
"Tunamshukuru Mungu kwa kutujaalia funga zetu katika kipindi cha mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kwani mwezi huu ni wa pekee kwa Waislamu duniani kote kufanya ibada, matendo ya huruma na kujitolea kwa ajili ya wengine, amesema Bw. Mombokaleo"
Pamoja na hayo ameshukuru Wadau wote na Wafanyakazi walioweza kuhudhuria hafla hiyo huku akisisitiza kwa kila mmoja kuendelea kuwa na ushirikiano ili kuweza kufikia malengo ya pamoja na kuwa mfano bora wa uongozi na utumishi katika jamii.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Awali Juma Fimbo akizungumza jambo wakati wa futari iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Abdul Mombokaleo akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa TAA, wadau mbalimbali wa viwanja vya ndege pamoja na wanafunzi kutoka kituo cha kulelea watoto cha Zili wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wadau mbalimbali wa viwanja vya ndege pamoja na wanafunzi kutoka kituo cha kulelea watoto cha Zili wakiwa kwenye wa hafla ya futari iliyoandaliwa na TAA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Awali Juma Fimbo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAA Abdul Mombokaleo wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi kutoka kituo cha kulelea watoto cha Zili wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo.
Picha za pamoja
No comments:
Post a Comment