ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 22, 2025

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE HARAMBEE


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini , Dkt. Frederick Shoo, kwenye Harambee ya ujenzi wa maktaba ya kisasa na ukumbi wa mkutano wa Seminari Ndogo ya Agape inayomilikiwa na Kanisa hilo iliyopo Moshi. Waziri Mkuu Kassim alimwakilisha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwenye Harambee hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini , Dkt. Frederick Shoo (kushoto) wakinadi chupa za kuhifadhia vimiminika katika Harambee ya ujenzi wa maktaba ya kisasa na ukumbi wa mkutano wa Seminari Ndogo ya Agape inayomilikiwa na Kanisa hilo iliyopo Moshi. Waziri Mkuu Kassim alimwakilisha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwenye Harambee hiyo iliyofanyia kwenye hoteli ya Serena jijini Dar eś salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akinadi saa iliyouzwa kwa sh. Mimilioni 4.4 katika Harambee ya ujenzi wa maktaba ya kisasa na ukumbi wa mkutano wa Seminari Ndogo ya Agape inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) iliyopo Moshi. Waziri Mkuu Kassim alimwakilisha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwenye Harambee hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Tuzo kwa naiba ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kumpongeza kwa kua mstari wa mbele katika kuchangia maboresho ya elimu kupitia ufadhili wa Rais SAMIA SCHOLARSHIP, kutoka kwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Frederick Shoo, kwenye Harambee ya ujenzi wa maktaba ya kisasa na ukumbi wa mkutano wa Seminari Ndogo ya Agape inayomilikiwa na Kanisa hilo iliyopo Moshi. Harambee hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia kwenye Harambee ya ujenzi wa maktaba ya kisasa na ukumbi wa mkutano wa Seminari Ndogo ya Agape inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), iliyopo Moshi. Waziri Mkuu Kassim alimwakilisha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwenye Harambee hiyo. Iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka kipaumbele kikubwa cha uwekezaji katika sekta ya elimu nchini ili kujenga jamii madhubuti, yenye kujitambua, kujitegemea, kujiheshimu na kufuata misingi ya uwajibikaji na ubunifu.

Ameyasema hayo alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika harambee ya ujenzi wa maktaba ya kisasa, ukumbi wa mikutano na madarasa ya amali ya shule ya Seminari ya Agape inayomilikiwa na Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini.

Katika harambee hiyo iliyofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo zaidi ya shilingi milioni 600 zilikusanywa ikiwa ni ahadi na fedha taslimu, Waziri Mkuu alisema sekta ya elimu ni wakala wa mabadiliko katika jamii kiuchumi, kiteknolojia na kiutamaduni katika kuleta maendeleo ya nchi.

“Harambee hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha kwamba tunafanya uwekezaji mkubwa katika elimu ya watoto wetu. Maktaba na madarasa ya amali katika Sekondari ya Agape yataleta manufaa mengi yenye tija kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.”

Alisema ni muhimu kutambua kwamba bila ya uwekezaji mzuri katika elimu, hatuwezi kufika mbali. “Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejizatiti kuunga mkono juhudi za taasisi mbalimbali zinazochangia katika ujenzi wa Taifa letu.”

Mheshimiwa Majaliwa amesema ili kuwa na vijana wenye maarifa na ujuzi wa kukabiliana na changamoto za kijamii, kitaifa na kimataifa inahitaji kuwa na sekta ya elimu iliyo bora, imara na inayokidhi mahitaji ya jamii.

Waziri Mkuu amesema ili kuongeza fursa za elimu kwa Watanzania wote, Serikali imeongeza idadi ya shule za msingi kutoka 16,656 mwaka 2020 hadi 19,783 mwaka 2024 na shule za sekondari kutoka 5,001 mwaka 2020 hadi 5,926 mwaka 2024.

Naye, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amelipongeza KKKT kwa kushirikiana na Serikali katika kuendeleza sekta ya elimu nchini.

Awali, Mhashamu Baba Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Shoo alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa kazi nzuri ya maboresho ya sekta ya elimu nchini. “Ninampongeza Mheshimiwa Rais Dkt Samia kwa maboresho ya sera ya elumu pamoja na ujenzi wa shule na ufadhili wa masomo ya sayansi.”

Akizungumzia kuhusu harambee hiyo alisema inalenga kukusanya shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya ujenzi maktaba ya kisasa, madarasa ya amali pamoja na ukumbi anuwai katika shule ya Seminari ya Agape ili kuunga mkono maboresho yaliyofanyika katika sera ya elimu.

No comments: