Afisa rasilimali watu wa NBAA Emmanuel Mfingwa akitoa salamu za Bodi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno wakati wa ziara ya masomo ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro waliotembelea Bodi hiyo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ya Bodi.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akiwakaribisha wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro waliotembelea Bodi hiyo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ya Bodi.
BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kutoa elimu/mafunzo kwa Vyuo vikuu pamoja na Shule za Sekondari ikiwa na lengo la kuwajengea ufahamu kuhusu shughuli mbalimbali za Bodi na kukuza taaluma ya Uhasibu.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo kwa niaba Mkurugenzi Mtendaji, Afisa rasilimali watu wa NBAA Emmanuel Mfingwa amesema si kila aliyesomea uhasibu anaweza kuwa Mhasibu bali inabidi kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili kupewa cheti cha kitaaluma ili uweze kutambulika kisheria kama Mhasibu na kuweza kufanya kazi nje na ndani ya nchi.
Aliongeza kuwa wanafunzi wa vyuo wa kozi nyingine tofauti na Uhasibu nao pia wana nafasi ya kufanya mitihani ya Bodi na hata wale wa sekondari waliomaliza kidato cha nne na sita wana nafasi pia ya kufanya mitihani hiyo alisema Mfingwa.
Naye mwalimu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro Iddi M Sudi ameishukuru Bodi kwa mwaliko wa wanafunzi ili kuja kupata Elimu ya Uhasibu.
Aliongeza kuwa wanachuo hao waliotembelea na kupata mafunzo hayo yatawapa dira na mwelekeo mzuri sasa na hapo baadae na pia aliwasisitiza wanachuo hao wakawe mabalozi kwa wenzao.
Afisa Udahili wa NBAA Naiman Fute akizungumza kuhusu namna wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro wanavyoweza kijisajili na kufanya mitihani ya Bodi pale watakapomaliza au wakiwa chuoni.
CPA Esther Masalla akiwasilisha mada kuhusu uanachama, jinsi ya kupanda daraja na usajili wa makampuni ya kihasibu na kikaguzi wakati wa ziara ya masomo ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro waliotembelea Bodi hiyo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ya Bodi.
CPA Yusuph Lema akitoa mada kuhusu misingi ya fedha kwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro
Mwakilishi wa wanafunzi wanaosoma masomo ya Uhasibu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro Benjamin Muusa Pili akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa NBAA kufuatia kufanikishwa kwa ziara yao katika ofisi hiyo
Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro Iddi M Sudi akitoa neno la shukrani kwa NBAA kwa niaba ya uongozi wa chuo hicho
Baadhi ya wanachuo wanaosoma masomo ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na wataalamu kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro wanaosoma masomo ya Uhasibu mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyofanyika katika ofisi za Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment