1. Fika muda na siku uliyoambiwa usichelewe hata dakika 5
Kesi yako inaweza kufutwa au kuondolewa dhamana.
2. Toa sauti kubwa unapozungumza
Inakera sana Hakimu/Jaji anapokusikia kwa chini na hutaki kuongeza sauti, kumbuka yeye ndie mtoa maamuzi.
3. Ongea kwa taratibu au kwa kituo.
Ili Hakimu au Jaji apate nafasi ya kuandika, kuwa speed itapelekea ushahidi wako muhimu kwa bahati mbaya unaweza usirekodiwe na kushindwa kesi.
4. Usiikasirikie Mahakama na kuzira.
Tumia maneno yenye hekima na ushawishi kujenga hoja zako.
5. Hakikisha unaushahidi kwa kila hoja unayojenga.
Maamuzi yanatokana na ushahidi zaidi kuliko maneno matupu.
6. Usiongee uongo.
Ukijulikana unadanganya hutoaminika tena
7. Epuka mapozi hasa wanawake.
Mahakamani ni sehemu serious sio sehemu ya kujishebedua na kuonyesha urembo
8. Usitoe Rushwa au kumpa Zawadi Hakimu au jaji.
Hasa kwenye dhamana au ili kushinda, ni kosa kisheria na unaweza kukamatwa on spot.
9. Usikatae kutoa ushahidi na kukaa kimya kwa kiburi unaweza pia kuchukuliwa hatua.
10. Mwisho Uhakimu na Ujaji ni kazi ya MUNGU aliyowapa watu wachache wenye MAADILI kufanya kwa niaba yake katika HAKI

No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake