ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 16, 2010

AJALI YA MOTO YAJERUHI WAFANYAKAZI MOROGORO

Hawa ni baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha Mavaza waliojeruhiwa katika ajali hiyo
NA DUNSTAN SHEKIDELE, MOROGORO
WAFANYAKAZI wa kiwanda cha MAVAZA kinachojihusisha na utengenezaji wa nguo za kisasa za michezo leo mchana wamejeruhiwa vibaya baada ya kiwanda hicho kupatwa na hitirafu ya umeme kwenye moja ya mashine za uzalishaji.
Wananchi wakijaribu kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi wa tukio hilo
Tukio hilo limetokea majira ya saa 9 alasiri na kwamba baada ya wafanyakazi hao kuona shoti hiyo ya umeme walianza kutimua mbio na kugombea kutoka nje ya kiwanda hicho ambapo msukumano wa kila mmoja akitaka kuinusulu roho yake ilisababisha wafanyakazi hao kukanyagana na kuumizana vibaya.
Mmoja wa majeruhi wa tukio hilo akiwa amebebwa kupelekwa hospitalini kupata matibabu
Moja wa wafanyakzi hao aliyenusulika katika janga hilo Bi Salma Ally alimueleza mwandishi wetu kwamba majira hayo ya saa 9 kiwanda hicho ambacho soko la vifaa vyake liko nchi za Ulaya na Marekeni lilipatwa na shoti hiyo ya umeme.

"Unajua kiwanda chetu kinawafanyakazi zaidi ya elufu 6 na kwamba majira ya saa tisa tuliona wenzetu wa sehemu ya uazlishaji wakitimua mbio huku wakilia na kusema kwamba kiwanda kinaungua, hivyo watu wa idara zote waliacha kazi na kugombea kutoka kiwandani na kwamba hali hiyo ya kugombea kutoka ndiyo iliyosababisha watu wengi kujeruhiwa na kwamba hatujui huko nyuma kama kuna wenzetu wamekufa au la" alisema Bi salma kwa uchungu.
Majeruhi wakiwaishwa hospitalini kupata huduma
Mwandshi wetu alishuhudia zaidi ya wafanyazi 60 wakifikishwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro huku wengi wao wakionekana kusumbuliwa na presha na wengine kuvunjika miguu.

Uongozi wa kiwanda hicho haukupatikana kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa bize na tukio hilo
MAELEZO NA PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS

No comments: