Advertisements

Friday, August 21, 2015

DALILI 10 ZA MKE/MPENZI ANAYEKUSALITI?

Dunia siku hizi imeharibika, wanawake nao ni mahodari wa kusaliti ndoa zao au mapenzi yao na wanaume hushindwa kuwagundua kwa sababu ya kutokuwa na muda mwingi wa kuwa nao.

Hii inatokea kwa sababu huenda muda mwingi uko kazini kwako na yeye kazini kwake au umemuacha nyumbani.
Sasa katika mazingira hayo utajuaje kama anakusaliti? Ni rahisi sana kama utanisoma kwa makini kwani hizi ndiyo dalili za mpenzi wa kike ambaye anakusaliti.

Haoneshi mapenzi anapokuwa na wewe

Wanawake wengi wanafanana katika kupenda, akimpenda mwanaume siyo rahisi kuficha hisia zake kwani huonesha hata pale anapokuwa na mpenzi wake kwa kumjali kumfanyia utundu wa hapa na pale.
Hata kutamani kuwa nawe kila wakati ni dalili moja wapo ya kukuonesha mapenzi, lakini ukimuona mwanamke wako hana ukaribu na wewe wala hajali uwepo au usiwepo, hiyo ni dalili kuwa ana mtu mwingine ambaye amempa nafasi.


2. Anapoteza mhemko faragha

Kwenye uhusiano mwanamke akiwa na mpenzi wake faragha huwa na mhemko wa hali ya juu, lakini ukiona amepoteza hali hiyo na hata ukiwa naye hainjoi, hii ni wazi kuwa ana mwanaume mwingine ambaye anaweza kumpa furaha hiyo.

3. Anaepuka kujifunga kwako

Wanawake wengi humpenda mwanaume ambaye atamuahidi ndoa na hupendelea kujifunga kwake hata anapompa majukumu ya kifamilia huyafanya ipasavyo, lakini ukimuona mwanamke anaepuka kujifunga kwako, jua huyo si wako bali ana mwingine ambaye anaamini ndiye atakuwa naye katika safari ya maisha.

4. Muda wote yupo bize

Unaweza kuwa unataka kumpeleka sehemu kwa maongezi, ukimuomba mtoke atakwambia yuko bize na ukijaribu kumuuliza ni kwa nini kila siku yuko bize atakujibu kuwa ni ubize tu.
Ukijaribu kuchati naye anakujibu baadaye sana au asikujibu kabisa. Ukimpigia hapokei, anakuja kukupigia baadaye na kukuambia alikuwa amebanwa.

5. Usiri wa kupitiliza

Ukiona mwanamke anakuwa msiri sana hata kwa vitu ambavyo alikuwa akikushirikisha moja kwa moja, jua tu huna nafasi tena kwake.

6. Hili la usmati nalo
Wanawake wengi hupendelea kuonekana smati sana pale anapojua atakutana na mpenzi wake au anapokuwa anatoka na mpenzi wake.

Ukiona mkeo au mpezi wako anavaa ovyo mkiwa mnatoka wote na akivaa vizuri ni pale anapotoka mwenyewe au na marafiki zake, wewe elewa tu kuwa huwa anamvalia mwenzako.

7. Simu yake anaweka password

Wanawake wengi si rahisi kuweka password kwenye simu zao kwa sababu mara nyingi ni wakweli na hasa akitokea kumpenda mwanaume humuachia wazi kila kitu ikiwa hata simu yake.
Ukiona mwanamke wako ameanza tabia ya kuweka password kwenye simu elewa kuna mwanaume anaye sasa hataki umfahamu.

8. Anakwepa maswali
Wanawake wengi hushindwa kuficha jambo kwa maana ni wakweli, ukitaka kumtega mhoji maswali mengi utamkamata kiurahisi, sasa ili kujiondoa kwenye kumjua atajitahidi kukwepa maswali.
Jitahidi kumbana kwa maswali mengi huku ukimuangalia usoni utaona jinsi atakavyokuwa mkali na majibu yake yatakuwa ni ya wasiwasi.

9. Malalamiko yanazidi

Iwapo utabaini malalamiko ya mpenzi wako kila siku hayana ukweli, jua moja kwa moja anatafuta pa’ kutokea. Huenda amepata mwanaume mpya hivyo anashindwa la kukwambia zaidi ya kukulalamikia ili hata akienda kwa huyo mwingine ujihisi umechangia.

10. Usipomtafuta hakuulizi

Mwanamke ukimkalia kimya kwa siku nzima bila kuongea naye au kumjulia hali kama ni mpenzi wako kweli au mumeo, huwa anaumia lakini ukiona anaona sawa na kukaa kimya jua ana mwanaume mwingine.
GPL

4 comments:

Unknown said...

It is true����

Unknown said...

Je mwanamke asieogopa kuingia ktk chumba cha mwanaume japo ni wanaishi hapo na hua anapewa tenda ya kufua nguo nae imekaaje mkuu

Unknown said...

Sahh

Anonymous said...

Duuu