ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 16, 2010

Machangudoa wafurahia kupatikana kwa dawa ya ukimwi Marekani

Baadhi ya Machangudoa wakiwa kazini
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Wanawake wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili yao [Machangudoa] wa mkoani hapa katikati ya wiki hii wamefurahia taarifa za kugundulika kwa tiba ya ugonjwa hatari wa Ukimwi unaochangia kwa kiasi kikubwa punguzo la pato la biashara yao hiyo.

Baadhi ya machangudoa hao waliozungumza na mwandishi wetu wamesema kwamba kupatikana kwa dawa hiyo ni ukombozi kwao kwa kuwa sehemu kubwa ya maisha yao wanategemea dili hilo la kuuza miili yao

"Mungu mkubwa katuletea ukombozi katika ishu yetu ambayo kimsingi haijawa rasmi lakini itatambulika duniani kote hivyo taarifa za kupatikana kwa dawa ya kutibu gonjwa hilo nchini marekani kwetu sisi ni faraja kubwa kwani tunaamini taarifa hizo zitaongeza kwa kiasi kikubwa pato la kazi yetu" alisema dada poa mmoja aliyekataa kutaja jina.

Wananchi wengi wa mkoani hapa wakiwemo machangudoa hao walionyesha furaha zao baada ya gazeti moja la kila siku kulipoti kwamba wanasayansi wa marekani kupitia Taasisi ya Magonjwa ya kuambukiza na mzio [Naida] wameutangazia ulimwengu kwamba taasisi yao hiyo imegundua dawa inayotibu Ukimwi kwa kiwango cha asilimia 99, bila chembe ya shaka lolote.

Muhudumu mmoja wa baa ya Makuti iliyopo maeneo ya Msamvu alimtonya Paparazi na kumueleza kwamba machanguoa wanojiuza katika baa hiyo katikati ya wiki iliyopita walifanya pati isiyo rasmi kwa kunywa pombe na nyama choma baada ya kupata taarifa kwamba dawa ya Ngoma imepatikana.

"Juzi machangu walifika hapa kwa maandamano wakitumia usafiri wa pikipiki baada ya kuwauliza walikuwa na sherehe gani mmoja wao alisema kwamba walikuwa sehemu wakijipongeza kwa kula nyama na pombe nyingi wakifurahia kugundulika kwa dawa ya ukimwi, mara baada ya kufika hapa huku wakiwa na gazeti lililoandika habari hizo waliendelea kunywa sambamba na kucheza muziki live uliokuwa ukipigwa na bendi ya hapa kwenye baa yetu" alisema muhudumu huyo wa kike ambaye alionekana dhahiri kuwachukia machangudoa hao.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu umebaini kwamba Mabaamedi wengi hawana mahusiano mazuri na machangudoa kwa kile kilichoonekana kwamba baadhi ya Mabaamedi wengi pia licha ya kufanya kazi za baa lakini hao hufanya kazi hiyo ya uchandu kwa kujilegeza kwa wateja wenye pesa.

Imeelzwa kwamba kitu kingine kilichowafurahisha machangudoa hao ni ile kauli wa serikali ya kusema kwamba itanunua dawa hizo na kuziingiza nchini hata kama zitauzwa bei ya juu kiasi gani.

Baadhi ya wananchi wengine waliohojiwa na mwandishi wetu walisema kwamba wananchi wa sibweteke na taarifa hizo na kujiachia katika uzinzi kwani kunamagonjwa kama malaria yana dawa lakini bado yanaondoa roho za watu.
MWISHO
CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS

No comments: