Rais Jakaya Kikwete, akihutubia Bunge mjini Dodoma jana wakati akihitimisha shughuli za Bunge la Tisa, ili kupisha nchakato wa uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.kushoto ni Spika wa Bunge Samwel Sitta
Waandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete ametaja kima cha chini cha mishahara ya watumishi wa umma kuwa ni Sh 135,000 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 107 tangu aingie madarakani mwaka 2005 alipokuta mshahara wa Sh65,000 kwa mwezi.Hili ni sawa na ongezeko la Sh31,000 kwenye mishahara ya kima cha chini ya Sh104,000 iliyokuwa ikilipwa na serikali kwa watuhimishi wa umma mwaka wa fedha ulioishia June 2010.
Rais kikwete aligusia kima hicho cha mishahara katika hotuba yake aliyoitoa jana bungeni wakati akilivunja rasmi bunge la tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuanza kwa Uchaguzi Mkuu.
Alisema ongezeko hilo la mishahara ni mafanikiwa makubwa kwa serikali yake ikilinganishwa na serikali zilizomtangulia.
"Katika kipindi hiki tumepandisha kima cha chini cha mishahara ya watumishi wa umma kutoka Sh 65,000 mwaka 2005 mpaka Sh 135,000 mwaka huu sawa na ongezeko la asilimia 107," alisema Rais Kikwete.KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment