Profesa Jwani Anthony Mwaikusa, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na majambazi mapema wiki hii, amezikwa jioni hii nyumbani kwake Mbezi Salasala na maziko yake kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji la Dar. Awali mwili wake uliagwa katika ukumbi wa Nkrumah Chuo Kikuu Dar na uongozi wa chuo kabla ya kupelekwa kwenye makazi yake ya milele. PICHANI: Mke wa marehemu akimuaga mume wake mpendwa katika ukumbi wa Nkrumah Chuo Kikuu cha Dar leo mchana.
Baadhi ya maprofesa wa UDSM aliowahi kufanyana nao kazi marehemu wakiwa mbele ya jeneza wakitoa heshima zao za mwisho
sehemu ya waombolezaji waliohudhuria ibada ya Nkrumah Hall mapema leo.
PICHA: Issa Mnally/GPL
No comments:
Post a Comment