ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 15, 2010

Dk Slaa arusha bomu kwa Sitta

Dk Wilbrod Slaa
Boniface Meena, Musoma
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa jana aligeuzia makombora yake kwa spika wa Bunge la Muungano, Samuel Sitta aliyeingia kwenye 'anga zake' baada ya kupinga sera ya wapinzani ya kutoa elimu bure akisema kuwa haiwezekani.“Sitta anajua hilo lakini unafiki ndiyo tatizo," alisema Dk Slaa wakati akihutubia mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Mukendo ulio Msoma Mjini.
Dk Slaa, ambaye amekuwa akitoa ahadi hiyo ya kutoa elimu bure iwapo Chadema itapewa ridhaa ya kuongoza nchi, alisema: "Fedha za Richmond na ufisadi mwingine uliofanyika zingeweza kuwa mwanzo wa elimu ya bure nchini.”
Spika Sitta, ambaye alikuwa akielezea wasiwasi wake dhidi ya njama za kumzuia kurudi bungeni, juzi alinukuliwa na vyombo vya habari akiponda wanasiasa wanaotoa ahadi ya elimu bure na kufuta kodi akisema kuwa hakuna serikali inayoendeshwa bila ya kutoza kodi na kwamba suala la kutoa elimu bure 

No comments: