ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 2, 2010

Helikopta kampeni ya Kikwete yagonga mti

Imetelekezwa Kisesa, Shinyanga
Zote tatu zimesajiliwa Afrika Kusini
WAKATI kukiwa na utata kuhusu zilikotoka helikopta zinazotumika katika kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, moja kati ya helikopta hizo imepata ajali mkoani Shinyanga, Raia Mwema limethibitishiwa.
Helkopta hiyo ZS-RPX, iliyosajiliwa Afrika Kusini, ilipata hitilifu juzi Jumatatu katika kijiji cha Mwandoya, yalipo makao makuu ya jimbo la Kisesa, wakati ikitua katika uwanja wa Shule ya Msingi Muungano.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia kutoka Shinyanga, helikopta hiyo ikiwa na marubani kutoka Afrika Kusini na ikitokea Bariadi, iligonga mti pembeni mwa uwanja wa Shule ya Muungano na kusababisha hitilafu katika mkia.
Imeelezwa kwamba mara baada ya kutokea kwa hitilafu hiyo, helikopta hiyo ilitua haraka na marubani hao kuchukuliwa na magari ya serikali kwenda mjini Meatu.
 
Hata hivyo, Rais Kikwete hakuwapo katika helikopta hiyo pamoja na kuwa tukio hilo liliathiri ratiba ya mgombea huyo ambaye aligusia katika mkutano wake wa hadhara katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Rais Kikwete aliwaomba radhi wakazi wa Shinyanga kwa kusema kwamba wamechelewa kufika mjini Shinyanga kutokana na ndege yake kupata hitilafu.

No comments: