Bw. John Murray McIntire akitoa ufafanuzi kuhusu misaada iliyotolewa na Benki ya Dunia tarehe 8/10/2010.
Mhe. Mustafa Haidi Mkulo, Waziri wa fedha na Uchumi akibadilishana mikataba aliyosaini na Bw. John Murray McIntire wa Benki ya Dunia.
Mhe. Mustafa Haidi Mkulo ambaye ni Waziri wa fedha na Uchumi na Bw. John Murray McIntire kwa pamoja wakisaini mikataba miwili ya mikopo yenye thamani ya kiasi cha shillingi bilioni 397.5.
Mhe. Mustafa Haidi Mkulo, Waziri wa fedha na Uchumi akishukuru kwa kufanikiwa kupata msaada huo wa kiasicha shilingi 397.5 kwa kipindi hiki kifupi alichokua hapa mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha na Uchumi Mhe. Mustafa Haidi Mkulo tarehe 8/10/2010 hapa mjini Washington-Dc amesaini mikataba miwili na Benki ya Dunia yenye thamani ya Dola za kimarekani Milioni 265, kiasi hicho ni sawa na shilingi za kitanzania bilioni 397.5.
Katika fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia, Dola za kimarekani million 115 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 172.5 zitatumika kugharamia bajeti ya serikali ya mwaka 2010/2011 na Dola za kimarekani million 150 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 225 zitatumika kugharamia mradi wa usambazaji umeme.
Aidha naye Bw. John Murray McIntire ambaye ni Mkurugenzi Mkazi kwa Nchi ya Tanzania, Uganda na Burundi.Aliipongeza Tanzania kwa kuwa makini katika matumizi ya fedha za misaada na kusema kuwa wamekubali kutoa fedha hizo kwa sababu ya juhudi ambazo wameziona. "Hii inaonyesha ni jinsi gani Tanzania inavyoweza kukabiliana na mtikisiko wa uchumi". alisema John.Alimalizia kwa kuwatakia Watanzania kazi njema na utekelezaji mwema wa miradi hiyo.
Naye Mhe. Mkulo baada ya kusaini mikataba hiyo aliwashukuru Benki ya Dunia kwa kusema kuwa," tunashukuru sana kwa kupatiwa misaada hii ambayo kwa kweli kwa nchi yetu ni faraja kubwa sana, tuta hakikisha misaada hii inatumika ipasavyo."
Aidha Mhe. Mkulo mapema wiki hii alisaini mikataba miwili na Benki ya Maendeleo ya Afrika yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 96.3 ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania bilioni 144.5
Katika fedha hizo zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kiasi cha shilingi bilioni 132.8 zitatumika kwenye mradi wa maji vijijini na kiasi cha shilingi bilioni 11.7 zitatumika kujenga uwezo kwa watumishi wa wizara ya Fedha na uchumi na Taasisi zake.
Jumla ya fedha zote zilizopatikana kwa ajili ya kuendeleza miradi kwa kipindi hiki kifupi cha mikutano ya mwaka ya shirikia la Fedha la kimataifa na kundi la Benki ya Dunia ni kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 542.0
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha na Uchumi.W
No comments:
Post a Comment