Selestina(shoto) na Jojo Jonathan
Familia ya Jojo na Selestina,Rashid Mkakile na Mkewe,wanatoa shukrani zao kwa wale wote waliohudhulia Misa ya mdogo wao Mpendwa,Marehemu Emmanuel Nzumbi Jonathan na ambao walishindwa kutokana na kutingwa na shughuli,tunajua nia ilikuwepo.
Pia tunapenda kuchukua nafasi hii kushukuru wote kwa faraja zenu na moyo wenu wa upendo,kusema ukweli mumetuonyesha mshimamano uliopo kati yetu Watanzania hasa tuishio mbali na Nyumbani na hii imeonyesha sisi ni kitu kimoja.
Tunatafuta neno au chochote kuwalipa kitakacholingana na wema,mshikamano,upendo na faraja mlizotupa lakini hatupati,kila neno halilingani na thamani ya yote mliotufanyia,sana sana tunaishia kusema asante sana na tunakuombeeni kwa Mwenyezi Mungu awazidishieni saba mara sabini
No comments:
Post a Comment