Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia tiketi ya Chadema, Mheshimiwa Joseph Osmund Mbilinyi ‘Mr II’ a.k.a Sugu, amezua vurugu ya aina yake baada ya mastaa wa Bongo kumgombea wakitaka kugonga nae snepu (kupiga naye picha).
Tukio hilo lilichukua nafasi katika Ukumbi wa TCC Chang’ombe, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ ilikuwa ikisugua kisigino.
Mhe. Sugu, akiwa na wapambe wake, Freddy Malick ‘Mkoloni’ na Issa Lupembe ‘Dr Levy’ alizama ukumbini humo majira ya ‘naiti’ kali ambapo alikwenda moja kwa zote na kuweka pozi jirani ya kaunta.
Kabla ya kuagiza chochote cha kupooza koo, Mheshimiwa alishangaa kuona mvua ya mastaa ikimmwagikia wakitaka japo kuuza naye sura kwenye picha, jambo lililozua tafrani kubwa huku wengine wakikanyagana.
Kwa upande wake Mheshimiwa ‘alimfinya’ mmoja wa mapaparazi walioukuwemo ndani ya ukumbi huo kuwa hali hiyo ilitokea kwasababu ni Mbunge na kama isingekuwa cheo hicho, mastaa hao wasingefanya hivyo.
Hata hivyo, baadhi ya mastaa walionekana wakitoka nje na walipoulizwa kulikoni, walisema kuwa mbona hata yeye alitoka nje ya Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete alipowahutubia wabunge wiki iliyopita.
CHANZO:DARHOTWIRE
No comments:
Post a Comment