PRINCE GEORGE'S MALL,MD
Jumanne ya Nov 23,2010 mida ya jioni nilikua katika pita pita zangu ndani ya Mall ya PG,mara niliingia duka maoja kuangalia uturi maana duka hilo usifika kwa kuuza uturi wa kila aina
Nilipokua ndani ya Duka mara nikasikia mzozo kati ya Dada Mmarekani mweusi akimuijia juu mhudumu anaechajisha bidhaa,mzozo ulikua mkubwa sana,na alisababisha msongamano wa watu,kilammoja wetu akitaka kujua kulikoni.
Kumbe Mdada wa Kinugu kaja juu mara baada ya yule Dada mhudumu kumtania kwamba Uturi ulionunua ameupenda na akamtania kwa kuonyesha dalili kama anataka kuuchukua,ndipo yule Dada wa kinugu akamwambia kama unaitaka we chukua nimekupa,muhudumu akamwambia nilikua nakutania tu,Yule Mdada akamwambia mhudumu nimekwambia huu uturi maadamu umeuomba mimi nimekupa.
Mhudumu hakuamini masikio yake,akamuuliza,unasema kweli au unatania?,Mdada aliendelea kusisistiza kauli yake nakwambia tene huu uturi nimekupati sihitaji pesa wala uturi,mhudumu akamwambia dada nilikua natania tu.
Dada wa Kinugu mwishowe akamuambia Muhudumu amwiite meneja wake,mhudumu aliposikia hayo naye kaja juu kwanini unamtaka meneja wakati nimekuambia huu uturi si uhitaji nilikua nakutania tu.
Hatimae meneja aliitwa kusuruhisha kizazaa hicho,mdada wa kinugu akamuelezea meneja kisa chote na meneja akamsikiliza mfanyakazi wake.
Ndipo meneja akaja na suluhisho akamuambia Dada wa kinugu,mfanyakazi wangu alikua anakutania na hivi ndivyo alivyo siku zote huchangamkia wateja.Mdada akarudia kauli yake akamuambia meneja sawa mimi nimempa huu uturi,meneja akamuuliza tena mdada wa kinugu unauhakika na maneno usemayo,mdada akasema ndio.
Meneja akachukua Uturi akampa mfanyakazi wake na kumuambia dada wa kinugu asante na kwa heri,ndpo yule Mdada kuondoka na meneja kumwambia mfanyakazi wake siku nyingine ikitokea kitu kama hiki huna haja ya kuniita wewe mteja kakususia kitu chake na wala hataki pesa yake ,chukua. Hapo ndipo niliposema hawa Wamarekani weusi wamezibuka.
No comments:
Post a Comment