ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 24, 2010

Polisi ilipowatia Polisi 12 mbaroni!

Polisi 12 jijini Dsm...wamelundikwa nyuma ya nondo (rumande) katika kituo cha polisi Chang’ombe, wakituhumiwa kwa hila wazi wazi kabisaaaaa za kuwakamata watuhumiwa na kuwaachia huru. 

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwakamata watu saba waliodaiwa kuiba mabomba na kumuua mlinzi wa Ghala la kiwanda cha United Builders Sultan Mohamed. 


Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke,David Misime amesema, tukio hilo lilitokea Novemba 16 mwaka huu katika ghala hilo lililoko katika barabara ya Nyerere, Dar es Salaam. 

Amesema, polisi wamewakamata polisi wenzao ili kuwahoji na iwapo itathibitika kuwa na kosa wanashitakiwa kwa taratibu za kijeshi. 

“Napenda kusisitiza kuwa polisi hawa hawakuhusika na wizi wa mabomba haya bali waliwakamata watuhumiwa hawa ambao ni wafanyabiashara na kuwaachia huru katika mazingira wanayoyafahamu wao hivyo tunaendelea kuwahoji ili kupata ukweli”amesema Misime. 

Amesema, wakati wakiwa doria, polisi hao 12 waliwakamata watuhumiwa saba ambao ni wafanyabiashara wa eneo la Mapambano lililoko katika wilaya hiyo ya Temeke wakitoka kwenye wizi wakiwa na mabomba hayo lakini waliwaachia huru. 

Misime amesema, polisi waliwakuta watuhumiwa wakiwa na mabomba hayo ambayo hutumika kujengea kwa ajili kushikilia zege hasa katika majengo kama maghorofa lakini waliwaachia huru. 

Baada ya kupata taarifa za wizi wa mabomba hayo walifanya uchunguzi na kugundua kuwa wezi hao walikamatwa na askari hao lakini wakaachiwa huru. 

Misime amesema, jeshi hilo liliwakamata watuhumiwa wakiwa na mabomba 161 ambayo polisi inayashikilia huku wakiendelea na upelelezi kwa kuwa inaonekana mabomba yaliyoibiwa ni zaidi ya hayo


                                   CHANZO:DARHOTWIRE .

No comments: