ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 27, 2010

Mwenzi wako anatoa harufu mbaya? Soma ujue jinsi ya ‘kuinjoi’ naye-3

Usafi wa mwili wako ni kitu ambacho msiri wa maisha yako anakihitaji. Hii ndiyo sababu ya kuandika mada hii kwa lengo la kuondoa manung’uniko, mikunjo na pengine ugomvi unaoweza kuepukika.


Nilikutaka utambue kuwa kitu kizuri ni kuanza kushughulikia usafi wako kabla ya ‘kudili’ na mwenzi wako. Si busara kuchonga mdomo kwa mwenzako, wakati wewe mwenyewe unahitaji msaada.

Umseme mwenzi wako kuwa anatoa harufu mbaya ya kwapa, vipi wewe unavyonuka mithili ya muhogo uliolala wiki tatu kwenye maji kwa sababu ya kuvaa nguo ya ndani ambayo haijakauka? Unafua na kuvaa mbichi (wash & wear).

Wiki iliyopita nilikomea kwenye uchambuzi wa nywele za faragha. Nikaeleza kwamba uwapo chumbani na mwenzi wako, bila shaka unahitaji huduma. Mwili umesisimka na akili yako inakwambia kwa wakati huo unahitaji kitu kimoja tu.

Kwamba huna kingine unachohitaji na ambacho kinaweza kutuliza ‘Wazaramo’ wako wanaokusumbua kichwani zaidi ya tunda la katikati. Bila shaka hicho ni kipengele maalum na huhitaji karaha ya aina yoyote.

Katika kipindi cha ‘romansi’, unagundua kuwa nywele zake za faragha zimesimama kama mtindo wa kiduku. Unanyong’onyea kwa maana hujafurahishwa kwa namna ulivyomkuta, lakini hiyo isikurudishe nyuma, una nafasi ya kufurahia zaidi mapenzi.

Tunapoangalia nywele za faragha, tunaangalia zile za kwapa na zile nyeti kabisa. Zote zina umuhimu wake katika utunzaji kwasababu zinaweza kukuaibisha wakati wowote endapo utashindwa kuzihudumia inavyotakiwa.
 
Kuhusu za kwapa inategemea uvumilivu wako lakini zile nyeti ni tatizo endapo utaamua kufumba macho na kumvaa hivyo hivyo. Kuhusika na mtu mwenye nywele nyingi za huko inaweza kukusababishia michubuko na maumivu makali.

Kuna hatari ya maradhi ya ngono (STD) na Ukimwi.
 Hata kama utatumia kondomu lakini nywele zake za faragha zitakuchubua kwasababu ni nyingi na kukusababishia maambukizi kwa njia ya damu au jasho kwa maana hazitakosekana uwapo mchezoni.

Kawaida mtu anapokuwa na nywele nyingi na harufu huwa kali kwasababu zina kawaida ya kuhifadhi jasho lenye mafuta, kwahiyo jukumu lako namba moja ni kuzinyoa ili kuondosha yote. Baada ya hapo utaona utamu wake.

Kuna njia ya kuzinyoa ambayo itafanya iwe sehemu mojawapo ya ‘romansi’, yaani wakati unamfanyia usafi wa nywele hizo, yeye anakuwa anaburudika na kusogeza hisia zake karibu.

Ukimuona anavyohangaika bila shaka nawe utavutika. Mapenzi mazuri sana.
Angalizo; Kuna wanaume wenye ugonjwa wa kulamba chumvi, wapo wanawake bila kufyonza lambalamba hawaoni kama sherehe imekamilika.

Wanawake nao wasipotembelewa mgodini kwa ulimi wanaona vibaya, vivyo hivyo wanaume.

Ipo wazi kwamba nywele za faragha zinaweza kuleta ugumu wa kuingia mgodini na kulamba chumvi. Ipo tahadhari ya uwepo wa bakteria eneo hilo, kwahiyo kupeleka ulimi ni hatari mara mia kwa mtu mwenye ‘mchicha’ mwingi.

ZINGATIA HATUA ZIFUATAZO
Una wembe au mashine safi? Kama ndivyo, basi baada ya kuona mwenzi wako ana hali hiyo, moja kwa moja andaa zana hizo kwa lengo la kumsafisha mpenzi wako. Usipompa huduma hiyo apewe na nani?

Muweke mkao unaotakiwa kisha chukua wembe wako msafi au mashine yenye makali ya kutosha. Chemsha maji ili wakati unakokotoa mchicha, kwa upande mwingine yawe yanapata moto.

Kuna watu hutumia dawa ya kunyolea nywele aina ya ‘magic’.
Wanakosea sana kwasababu baada ya kutumia kwa muda, kemikali zake husababisha madhara kwenye njia ya mkojo. Hivyo basi, usimnyoe mwenzi wako kwa ‘magic’.

Utulivu wako ni muhimu! Nyoa taratibu ili usimchanje hovyo, pia kusogeza hisia zake karibu. Ukishamaliza, chukua maji ya moto lakini siyo ya kuunguza, kisha msafishe kikamilifu kwa kutumia kitambaa laini.

Huduma hiyo utakayompa, itampeleka sayari nyingine. Na ukishamaliza hilo unaweza kuunganisha na ile shughuli iliyokusudiwa. Utaona ni jambo dogo lakini kwenye mapenzi ni kubwa. Tekeleza uone faida yake.

Kwa usafi huo, hapo hata chumvi unaweza kulamba, lambalamba unaweza kufyonza bila bughudha ya aina yoyoye. Ukifanya hayo, utaona jinsi mapenzi yalivyo matamu. Ukumbi ni wako sasa.

Kuhusu nywele za kwapa, hatua ni hizo hizo, mnyoe taratibu kisha tumia maji ya uvuguvugu kumsafisha huku ukimkanda kanda taratibu.

Hilo ni eneo makini, ukimfanya hivyo utamsisimua, hisia zake utazileta jirani yako.
Tukutane wiki ijayo kujadili usafi zaidi.

No comments: