ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 4, 2010

Tohara Ya ‘Lazima’ Kwa Wanaume Yaja



KUTOKANA na utafiti wa kisayansi kuonesha kuwa kutofanya tohara kwawanaume ni moja ya sababu zinazochangia maambukizi ya Ukimwi, wanaumekatika mikoa saba nchini wanatarajiwa kufanyiwa tohara kuanzia mwakanikwa sababu inayo idadi kubwa ya wanaume wasiotahiriwa.



Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema itaanza operesheni maalumukwa kushirikiana na wadau wengine yakiwemo mashirika ya misaada kutokaMarekani, kufanya tohara kwa wanaume hao katika mikoa ya Mbeya,Iringa, Rukwa, Kagera, Tabora, Shinyanga na Wilaya ya Rorya mkoaniMara.


Hayo yalibainishwa na Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Haji Mponda, janamjini hapa, katika hotuba yake kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi yaWaziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kumkaribishaMakamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal kuhitimisha maadhimisho yaSiku ya Ukimwi Duniani, Kitaifa mjini hapa.


Dk. Mponda alisema utafiti uliofanyika na taasisi mbalimbalizinazojihusisha na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi,imeonesha kuwa mikoa hiyo inaongoza kwa maambukizi na moja ya sababuni kuwepo kwa idadi mkubwa ya wanaume wasiofanyiwa tohara.“Mpango wa Wizara ni kutaka kupunguza kiwango cha maambukizi ya VVU nautafiti umeonesha mikoa hii ina idadi ndogo ya wanaume waliofanyiwatohara, lakini ina viwango vya juu vya maambukizi,” alisema Wazirihuyo.


Hivyo alisema mpango wa Wizara ambao tayari ulianza kwa majaribiokatika mikoa ya Iringa, Mbeya na Kagera, itaendelezwa zaidi katikamikoa iliyoainishwa kuanzia mwakani kwa ufadhili wa Serikali yaMarekani kupitia mashirika yao ya misaada sambamba na marafiki wenginewa maendeleo.Alisema mpango huo wa kuwafanyia tohara wanaume katika mikoa hiyoumelenga kuwafikia wanaume zaidi ya milioni 2.5 na wanaume wa mikoahiyo wameonesha kufurahishwa na uamuzi huo wa kuwatahiri.


Katika takwimu zilizotolewa na TACAIDS ya viwango vya maambukizi yaVVU ya mwaka 2003/ 2004, Mkoa wa Iringa ulikuwa na maambukizi yaasilimia 13.4 ambapo kwa mwaka 2007/2008 maambukizi ni asilimia 15.7.Mkoa wa Mara kwa miaka hiyo, maambukizi yalikuwa ni asilimia 3.5 nakuongezeka mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 7.7 wakati Mkoa waShinyanga maambukizi yalikuwa ni asilimia 6.5 ambapo kwa mwaka2007/2008 viwango vya maambukizi ni asilimia 7.4.Naye Mwandishi Wetu, Flora Mwakasala anaripoti kuwa Kaimu Mkuu wa Mkoawa Dar es Salaam, Chiku Galawa ametaka mabango yote ya waganga wa jadiyanayotangaza kuwepo kwa dawa za kuongeza nguvu za kiume, yaondolewekwa kuwa ni kichocheo cha ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.


Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi yaliyofanyika janakimkoa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Galawa alisema mabango hayoyamebandikwa mitaani kwa wingi.“Huu ni utapeli mkubwa, nani kasema watu wanahitaji kuongezewa nguvuza kiume? Jambo hili ni sawa na kuwahamasisha watu waendelee kufanyauasherati na kuongeza maambukizi mapya ya VVU,” alisema.Alisema kitendo cha watu kuongeza nguvu za kiume kinawashawishikuendelea kufanya ngono, jambo linalosababisha kuwepo kwa ongezekokubwa la maambukizi hasa kwa vijana ambao ni taifa la kesho.“Tutashirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa Serikali za Mitaakuhakikisha mabango yote yaliyobandikwa mitaani na barabaraniyanaondolewa,” alisema.


Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa MafunzoTaifa wa Chama cha Waganga wa Tiba za Asili, Sadick Kalimaunga alisemakauli hiyo ya Galawa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, si sahihi kwakuwa kazi yao ni kuwasaidia wanaume wenye matatizo ya upungufu wanguvu za kiume.“Sisi hatuchochei maambukizi ya VVU kama wanavyodai bali tunawasaidiawanaume wenye matatizo hayo kudumisha ndoa zao kwa kuwaongezea nguvuza kiume ili waweze kufanya tendo hilo kikamilifu,” alisema.Aidha, alisema kitendo cha Serikali kuondoa mabango hayo kitasababishabaadhi ya watu wanaohitaji tiba hizo ambazo zilikuwepo tangu enzikukosa huduma na wengine ndoa zao kuvunjika.Kwa mujibu wa takwimu, Dar es Salaam ni mkoa unaoshika nafasi ya pilinchini kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU cha asilimia9.3. Iringa inaongozwa kwa kuwa na asilimia 15.7.

No comments: