ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 27, 2011

UN yamwekea vikwazo Gaddafi-BBC

UN
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura - na kupita bila kupingwa - ya kuuwekea vikwazo utawala wa Muammar Gaddafi kutokana na hatua yake ya kutaka kuzima maandamano.
Baraza hilo limeunga mkono kuweka vikwazo vya silaha na kupiga tanji amana, huku wakifikisha suala hilo katika Mahakama ya Kimataifa (ICC) kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinaadamu.
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kiongozi huyo wa Libya aondoke madarakani na kuondoka nchini humo.

Serikali ya mpito

Hata hivyo bado anadhibiti mji wa Tripoli, lakini upande wa mashariki wa nchi unashikiliwa na waadamanaji.
Majadiliano ya kuunda serikali ya mpito ya wanaompinga Gaddafi inaarifiwa yanafanyika.
Mustafa Abdel-Jalil, aliyejiuzulu uwaziri wa sheria kwa kupinga matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji amesema tume yenye raia na wanajeshi itaandaa uchaguzi katika kipindi cha miezi mitatu, limekaririwa gazeti binafsi Quryna.
Libya
Waandamanaji Benghazi
Mabalozi wa Libya nchini Marekani na katika Umoja wa Mataifa wameunga mkono mpango huo, ambao unajadiliwa katika mji wa mashariki unaodhibitiwa na waasi wa Benghazi.
Umoja wa Mataifa (UN) unakadiria kuwa zaidi ya watu 1,000 wamekufa, wakati utawala wa Kanali Gaddafi ukijitahidi kuzima vuguvugu la mabadiliko lililodumu kwa siku kumi.
Hii ni mara ya pili tu kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufikisha nchi katika ICC, na ni kwa mara ya kwanza kura kama hiyo kupita bila kupingwa.

No comments: