Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande (Mb), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) uliofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Prof. Sylvia S. Temu akizungumza na kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi uliyofanyika APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya NBAA wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande (Mb) wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) uliyofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), uliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya NBAA CPA Issa Masoud akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande (Mb) mara baada ya kuzindua Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)
Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande (Mb)(katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wapya wa Bodi walioteuliwa. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo CPA Prof. Sylvia S. Temu akifuatiwa na CPA Fredrick Msumali(Mjumbe wa Bodi). Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno, akifuatiwa na CPA Leonard Mkude (Mjumbe wa Bodi). Waliosimama kutoka kushoto ni CPA Paul Bilabaye, CPA Aisha Kapande, CPA John Ndetico, CPA Salhina Mkumba, CPA Mwamini Tuli na CPA Issa Masoud wote ni wajumbe wa Bodi
Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande (Mb)(katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi na Menejimeti ya NBAA
Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande (Mb)(katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa APC Hotel and Conference Center Bunju jijini Dar es Salaam ulipofanyika uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA.
Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande (Mb) ameitaka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano kwa kuhakikisha inapitia mitaala iliyopo kwa ajili ya uboreshaji wa Taaluma ya uhasibu ili iweze kutoa mchango katika kukuza uchumi.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande (Mb) wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), iliyofanyika tarehe 18 Disemba, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano-APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Chande amesema kazi ya wakurugenzi wapya wa Bodi walioteuliwa ni kukuza na kuendeleza mafanikio na mpango mkakati wa shirika ulioundwa na kufanya mapitio ya mara kwa mara.
Aidha ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha inasimamia vyema ujenzi wa ofisi ya NBAA katika makao makuu ya nchi Dodoma.
"Kwa wakati huu wa mabadiliko ya kibiashara tumeshuhudia ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. Malengo ya serikali ya awamu ya sita ni kuendelea na kukuza uchumi wa nchi na taaluma hii ya Uhasibu ina mchango mkubwa katika kufanikisha hilo, hivyo basi kwa wajumbe mlioteuliwa, yawapasa kufanya kazi huku mkizingatia malengo ya Taifa." Alisema Chande
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA CPA Prof. Sylvia Temu amesema wao kama bodi watahakikisha wanafanya kazi ya kusimamia na kukuza tasnia ya uhasibu na Ukaguzi hapa nchini ili iweze kutoa huduma stahiki
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Pius Maneno ametoa shukrani kwa Naibu Waziri kwa kuzindua Bodi ya Wakurugenzi ya NBAA.
No comments:
Post a Comment