ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 4, 2011

Uteuzi uliofanywa na Kibaki kinyume cha katiba -Mahakama kuu-VOA

Rais Mwai Kibaki wa Kenya akihutubia kikao cha ufunguzi cha bunge la Kenya.
Mahakama kuu ya Kenya imetoa uamuzi kuwa utaratibu alotumia Rais Mwai Kibaki kuwateua maafisa wanne wa sekta ya sheria na fedha ulikuwa ni kinyume cha katiba.
Mahakama kuu imeamuru kufutiliwa mbali uteuzi huo baada ya kusikiliza kesi iliyowasilishwa kulalamika juu ya uhalali wa hatua hiyo.
Hapo January 28, 2011 Rais Kibaki alimteua jaji wa mahakama ya kukata rufaa Alnashr Visram kuwa Jaji Mkuu wa serikali, naye Profesa Githu Muigsai aliteuliwa kama mwanasheria mkuu, Kioko Kilukumi mwendesha mashitaka mkuu na William Kirwa mkuu wa bajeti.
Wakati huo huo Spika wa bunge la Kenya, Kenneth Marende alishindwa kuamua juu ya kuwasilisha hoja ya  kuidhinisha majina ya maafisa hao wapya, kufuatia uwamuzi wa Mahakama Kuu.

No comments: