ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 2, 2011

Wapinzani wazuia shambulio la Gaddafi

Gaddafi
Wapinzani wamepigana kuzuia wanajeshi wanaomtii Kanali Muammar Gaddafi kuuchukua tena mji wa mashariki wa Brega.
Majeshi ya Gaddafi yaliingia katika maeneo ya mashariki kwa mara ya kwanza tangu mji huo uchukuliwe na waandamanaji wiki mbili zilizopita.
Mwandishi wa BBC John Simpson aliyepo Brega anasema wanajeshi wanaomtii Gaddafi hawaonekani kwa sasa mjini humo.

Mapema Kanali Gaddafi alisema kupitia televisheni kuwa "atapigana hadi dakika ya mwisho" na kuonya kuwa maelfu ya wananchi wa Libya watakufa iwapo majeshi ya nchi za Mashariki yataingilia kati.
Mwandishi wetu almefika katika chuo kikuu cha Brega, ambako mapigano makali yalitokea, na inaonekana kuwa wanajeshi wa Gaddafi hawapo kabisa.
Alisema afisa wa juu wa kundi la wanaopinga utawala wa Gaddafi alisema majeshi ya Gaddafi huenda yakawa yameishiwa risasi na kulazimika kurudi nyuma.
Waandamanaji hao wameonekana kufurahia na kujivunia walichofanikisha, anasema mwandishi wetu, na hali katika mji huo ni kama watu wa Kanali Gaddafi hawana hamasa kubwa na kazi wanayoifanya.

No comments: