ROME, Italia
RAIS wa klabu ya Palermo, Maurizio Zamparini ameiambia Chelsea haitaweza kumchukua kiungo Javier Pastore kutoka katika klabu hiyo bila kuwa na dola 44 milioni.Zamparini alisema klabu za Chelsea, Real Madrid, Manchester City na Barcelona zote zinamtaka kiungo huyo mshambuliaji ambaye ni raia wa Argentina.

"Nimemuambia wakala wake aangalie soko zuri la mchezaji huyo na mpaka sasa ameishafanya hivyo na tunatarajia mwisho wa wiki tutakaa na kuangalia tumuuze katika klabu ipi mchezaji huyo kwa ajili ya maisha yake ya baadaye,"alisema Zamparini.
Zamparini aliongeza kuwa wiki iliyopita alikataa dau la klabu ya Chelsea ambayo imeonyesha kumhitaji Pastore ambaye ana miaka 22.Pastore alijiunga na klabu ya Palermo miaka miwili iliyopita kwa kiasi cha pauni 5 milioni na alikuwepo katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kilichoshiriki Fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini mwaka jana.
Pia zipo taarifa hata klabu ya Manchester United na yenyewe inamuhitaji mchezaji huyo.Wakati huo huo klabu ya Chelsea pia inaonekana inaelekea kumkosa Neymar ambaye walikuwa wakimuhitaji muda mrefu.
Neymar,19, hivi sasa mipango yake ipo katika kuhakikisha anajiunga na klabu ya Real Madrid.Wakala mkubwa Ernesto Bronzetti ambaye ni rafiki wa karibu na raisi wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez alinukuliwa akisema hatua nyingi zimeishafanyika katika kuhakikisha Neymar anajiunga na Real Madrid.
Inavyooneka kitendo cha Chelsea kuteua kocha ambaye atachukua kazi ya kocha Carlo Ancelotti ambaye walimtimua kinaathiri timu hiyo hivi sasa katika kuhakikisha inapata wachezaji bora.
No comments:
Post a Comment