ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 23, 2011

Katika usaliti;muda, giza si kigezo-3-GPL

“Wanawake wa hivi, katika kumi, sita si waaminifu kwani hutumia nafasi hiyo kufanya usaliti na kujiweka sawa, akirudi nyumbani anakuwa ‘safi’. 
Johannes anasema haoni sababu ya wanawake kubeba vitu vyote hivyo kwa kisingizio cha ‘wanawake wana mambo mengi.’
Sasa tuendelee…

IMANI YA WANAUME KWA WENZA WAO
Kifupi, mambo aliyoyasema Johannes yana maana kwa upande mmoja au mwingine kwani siku zote, wanaume wamekuwa wakilalamikia tabia za wake au wapenzi wao kubeba ‘dressing table’ yote kwenye mkoba.


Wanaume wanaamini kuwa, tabia hiyo inaweza kuwafanya wakasaliti na kurudi nyumbani wakiwa safi kama walivyotoka asubuhi.

WANAWAKE WAFANYAKAZI HATARI ZAIDI?
Hili linaungwa mkono na Jane Misogi wa Mwananyamala jijini Dar.
Yeye anasema kuwa, aliwahi kugundua kuwa, kati ya wanawake na wanaume, wanawake wanasaliti sana wenzao nyakati za asubuhi hadi jioni.

Jane akaongeza kwamba, baadhi ya wanawake wanabeba khanga, kioo na vipodozi vingine kwa makusudi kabisa, wakiingia gesti wakitoka wanakuwa kama hawajalala kwenye kitanda.
Alisema hakatai wanawake kuwa na vipodozi kwenye mikoba kwani wanatakiwa kuwa safi muda wote, lakini akasema si vizuri kusaliti.

Hapa anashuhudia: “Kuna kaka yangu alikuwa na mke anayefanya kazi. Kila asubuhi akitoka begi limejaa vipodozi, kitenge, khanga, kandambili mpaka sendozi. Mumewe alikuwa akishangaa sana, lakini alikuwa akitumia busara kutomuuliza.

“Siku moja, baadhi ya marafiki zake katika maongezi yao walizungumzia tabia ya wanawake wa hivyo, kaka akashituka pale na kuanza kumfuatili mkewe.
Kuna siku, mke aliporudi jioni kutoka kazini, kaka akavizia wakati hayupo chumbani akafungua mkoba wake.

“Ndani ya mkoba huo akakuta kitenge kikiwa kimelowa maji, akashangaa sana. Akafukua tena na kukuta ‘kufuli’ mbichi yaani ikiwa imetoka kufuliwa.
“Alipozidi kupekua akakumbana na sabuni ya kuogea mpya ambayo hata pale nyumbani ilikuwepo, ikiwa imetumika mara moja.

“Alimbana sana mkewe hadi ikafika mahali akakiri kutoka kazini. Tena hapo ni baada ya kumtishia talaka, akasema ni kweli alikuwa gesti na mwanamume ambaye wanafanya kazi wote ofisini moja.”

MWANAMKE, MWANAMUME NANI MSALITI ZAIDI?
Unaona, hapa kuna kitu cha kujifunza kwamba, mume alikuwa akimwamini mkewe kwani akitoka asubuhi kwenda kazini, saa kumi na moja amesharudi kumbe akitoka saa tisa anapitia kwanza gesti na kufanya uchafu wake, kwa hiyo muda, giza si kigezo.

Miaka ya hivi karibuni, wana ndoa au wamepenzi wamejifunza kwamba, hakuna haja ya kutumia giza kusaliti wenza wao kwanza wakati huo wapenzi wao wanakuwa wanasumbua kwa simu za ‘uko wapi?’
Kwa hiyo wanachofanya ‘wezi’ hawa ili wale taratibu wanasaliti nyakati za asubuhi, mchana au alasiri ambapo wenza wao wanakuwa bize na majukumu mengine.

Katika kitabu cha Love is Poison cha Christian Lures cha hivi karibuni kinasema kwamba, utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa, asilimia 65 ya wanawake wanasiliti mchana, asilimia 50 ya wanaume wanasaliti usiku.

Aidha, kwa mujibu wa kitabu hicho hicho, katika kila wanawake 100, 75 huenda mbali na maeneo wanayoishi ili kusaliti wakati katika kila wanaume 100, 50 tu ndiyo wanaopenda kwenda mbali kusaliti.

Utafiti huo umekwenda mbali zaidi pale ulipobaini kuwa, maisha ya sasa, katika kila wanaume 100 walio kwenye ndoa, 85 wana wapenzi nje, wakati katika wanawake 100, 75 ndiyo wana wapenzi nje.
Hii namba inatisha sana, lakini miongoni mwao sasa ndiyo wanapatikana wale wanaosaliti mchana.

KWANINI WANAWAKE WANASALITI MCHANA?
Utafiti wa kawaida kabisa umethibitisha kuwa, wanawake wengi wanasaliti mchana kwa sababu kuanzia saa moja jioni na kuendelea wanakuwa na majukumu ya lazima ya familia.
Si rahisi mama anayesubiriwa na watoto wake nyumbani akafanya upuuzi wake muda huo kwani baba naye akirudi usiku anataka kukuta chakula na mambo mengine yote yakiwa yamefanyika kwa usahihi. Tukutane wiki ijayo na mada yetu hii.

No comments: