Hawa Mathias, Mbeya
POLISI mkoani Mbeya, wanamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Hasamba, wilayani Mbozi, kwa tuhuma za kukutwa na kiganja cha mkono wa mtoto mchanga.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, alisema mtuhumiwa alikamatwa mchana wa Juni 22 mwaka huu.

"Kukamatwa kwa mtu huyo kulikuja baada ya polisi kupata taarifa kwamba raia wema wamweka chini ya ulinzi mtu huyo akiwa na kiganja cha mkono wa kushoto. Kilikuwa ndani ya ndoo ya maji ambayo aliificha ndani ya nyumba yake," alisema.
Kamanda Nyombi alisema walipofika nyumbani kwa mtuhumiwa,polisi walifanikiwa kuipata ndoo iliyokuwa imetumika kuhifadhia kiganja hicho na kwamba ilikuwa imefichwa nyuma la mlango.Nyombi alisema haikuweza kufahamika mara moja kama kiganja hicho ni cha mtoto hai au mfu na kwamba polisi wanaendelea na uchungunzi.
Kamanda huyo alisema uchunguzi huo ukikamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.Nyombi alisema kiganja hicho kimehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi ya Vwawa, kwa uchunguzi zaidi.
Aliwaomba wananchi waendelee kushirikiana na polisi katika kuwafichua watu wanaojihusisha na matukio ya uhalifu, ili sheria ichukue mkondo wake.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment