ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 12, 2011

Mechi kati ya DC Nyalugusu na Bongo Real
Luka Kinyang'anyiro lawamani,
mchezo wavunjika dkk 90
Tanzania one(Alawi) Nyota wa mchezo
Adam akiwa na mchua msuli wake
Timu ya Bongo Real
Timu ya DC Nyalugusu 
Mechi kati ya DC Nyalugusu na Bongo Real umevunjika mnako dakika ya 90 huku Bongo Real wakiwa mbele kwa Bao 3-2.

Mechi hiyo ya kukata na shoka ambayo ilikua imepaniwa zaidi na DC Nyalugusu ambao waliingia uwanjani hapo kwa mbwembwe za uzi mpya rangi nyekundu bukta nyeusi huku wakiwatolea maneno ya kejeli wapinzani wao wa Bongo Real kwamba haina uwezo wa kununua jezi na hawana uwezo wa kusajili wachezaji wapya.
Maneno hayo yalizihirishwa pale uwanjani na DC Nyalugusu walipoingia na wachezaji walikua wakiichezea Bongo Real,Libe,Vincent na Beach Boy wakidai kwamba wamewanunua kwa bei mbaya,kabla ya mechi hiyo wachezaji hao walikua wamekubali kuichezea Bongo Real.kwenye mpambano huo.


Mchezo ulianza kwa DC Nyalugusu kulishambulia goli la Bongo Real kama nyuki huku beki ya Bongo Real ikiongozwa na kipa wao,Tanzania One,Alawi ikifanya kazi ya ziada kuokoa hatari zote zinazoekelekea golini hapo.
Kizingiti kikubwa cha DC Nyalugusu kilikua golikipa Tanzania One ambae kwenye mechi hii ndie alikua nyota ya mchezo kwani aliokoa mipira mingi iliyokua ikiekea nyavuni.

Na kama si kasoro za refarii Kenyata kuonekana kuipendelea DC Nyalugusu,mechi hii ingekua nzuri sana kwani upinzani ulikua mkali na mtanange ulikuwa wa kusisimua,kwani DC Nyalugusu walikua wakitandaza mpira wakitabuni tatizo ilikua umaliziaji na hii ni kwa sababu ukuta na golikipa wa Bongo Real walitumia akili sana na wachezaji wake ni wazoefu wa mechi kama zile.
kunako dakika ya 32 mchezaji wingi wa kushoto Abuu aliipatia Bongo Real bao la kuongoza baada ya kutokea kigugumizi cha mabeki wa DC Nyalugusu walipotaka kuokoa pasi ndefu iliyopigwa na Adam NY ambae mechi hii amecheza kama kiuongo wa juu kawaida hucheza kama beki wa kati.

Bao hilo liliwafanya DC Nyalugusu kulishambulia goli la wapinzani wao kama nyuki na kunako dakika ya 37 Vincent aliandika bao safi la kusawazisha kwa kuwazidi mabeki wa Bongo Real ujanja na kutumbukiza mpira kimiani kwa bao la kushutukiza huku mabeki wakifikiri angetoa pasi.

Mpaka mapunziko Bongo Real ilikua mbele kwa bao 3-1, bao la 2 lililofungwa kunako dkk ya 42 na Seif kwa kiki ya nje ya 18 iliyopigwa kifundi kwa kugonga posti ya kulia na kumfanya Kipa wa DC Nyalugusu asijue la kufanya na kunako dakika ya 44.Adam NY aliifungia Bongo Real Bao la 3 kwa mpira wa adhabu alioupiga kutoka mita 30 na kuingia moja kwa moja nyavu ndogo.

Kipindi cha pili kilianza kwa DC Nyalugusu kufanya mabadiliko ya kumtoa kipa wao aliyeanza na kmuingiza kipa wa pili na kuanza kipindi hicho cha lala unono kwa kulishambulia goli la Bongo Real kama nyati aliejeruhiwa.

Mashambulizi hayo yalizaa matunda kunako dakika ya 79 wakati Jabiri Jongo alipoipatia DC Nyalugusu bao la pili kwa kumalizia mpira uliopigwa kutoka winga ya kulia na Vincent huku mabeki wa Bongo Real wakizani Vincent alikua amejenga kibanda cha muda kabala hajapokea pasi toka kwa Libe.

Lawama zidi ya Refa zilizidi pale Abuu alipokwatuliwa ndani ya 18 na Refa Kenyata kupeta kitendo hicho kilizidi kuwatia hasira benchi la Bongo Real.

Kunako dakika ya 90 kulitokea piga nipige golini mwa Bongo Real  na kwa mshangao wa wengi Refa alipuliza kipenga kuashiria penati kwa madai beki wa Bongo Real aliunawa mpira uliopigwa na Vincent ndani ya 18,penati hiyo iligomewa na Bongo Real huku wachezaji na benchi la DC Nyalugusu wakimshutumu  Luka Kinyang'anyiro mchezaji wa Bongo Real kwamba yeye ndio amesababisha wachezaji kugomea penati na kuwashawishi watoke nje ya uwanja.

Kitendo hicho cha wachezaji wa Bongo Real kugomea kuendelea na mchezo killizidi kuwatibua DC Nyalugusu na kuanza kmsemea Ovyo Luka Kinyang'anyiro.

Luka Kinyang'anyiro amekubali kubeba lawama zote za kuvunjika kwa mechi hiyo mradi tu,DC Nyalugusu wamelalanacho 3-2 na timu kapteni wa Bongo Real Richard Mawenya amesema kama DC Nyalugusu wanataka mechi ya marudiano lazima watulipe $10,000 ndio tutakubali kucheza nao amasivyo wataendelea kulala unono nacho 3-2.

1 comment:

Ms Dida said...

Du si mchezo DC mnaendeleza mtanange sana nawajua sana hawa wachezaji LIBE, VICENT NA BEACH BOY hawa watu mpira wamecheza na najua walikuja boston walipiga sana mtanange na timu ya boston safi sana muendeleze libeneke salute DC NYARUGUSU na Bongo Real.