ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 20, 2011

Michelle Obama safarini Afrika kusini-VOA

Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama
Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama anaelekea Afrika kusini ambako anaanza ziara yake ya siku tano katika bara hilo akilenga masuala ya  vijana na uongozi, elimu, afya na mazoezi.

Mke wa rais wa marekani, barack Obama atawasili katika mji mkuu Pretoria Jumatatu ambapo atakutana na Rais wa Afrika kusini, Jacob Zuma.
Michelle pia anatarajiwa kwenda  Johannesburg kutembelea taasisi ya Mandela pamoja na pia makumbusho ya ubaguzi mjini humo.

Bibi Obama atahutubia kwenye mkutano wa  wanawake vijana kutoka nchini za Afrika zilizo chini ya jangwa la  Sahara zilizohusika katika juhudi za jamii na uchumi katika nchi zao. Mkutano huo umefadhili na Marekani.
Michelle pia atakutana na mchungaji Desmond Tutu na mashirika yanayopambana na HIV na ukimwi nchini Afrika kusini.

Bibi Obama atakamilisha safari  yake kwa ziara ya siku mbili nchini Botswana. Mke wa Rais ameongozana na mama yake mzazi na watoto wake wa kike, Malia na Sasha.

No comments: