ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 11, 2011

Hii Kweli Ni Utu Muhimbili???

Na Elle Ruger
Hatuna haja ya kuwa kama wenzetu wa Misri au Libya, ila leo nimeamua kuwa Mtanzania tofauti kidogo:mwenye kuanzisha majadiliano ili kinacho nilalamisha kipatiwe utatuzi.  Ninaamini mkiishasoma mtagundua siko pekee yangu mwenye uchungu na huzuni na hasira kuhusu hali ya Muhimbili na utu wa wagonjwa.Wanasema waTanzania kazi yetu ni kulalamika weee bila kufanya kitu chochote kubadilisha hali inayotufanya tulalamike.

Mfano wangu ni wa wadi ya Sewahaji (18), samahani sijui majina vizuri ya wadi za Muhimbili.  Nina uhakika kabisa kwamba Sewahaji hali ni mbaya sana.  Hamna utu wala heshima.
Niliona wadi imejaa tokea ubarazani kabla hata ya kuingia wadini.  Kuna wagonjwa sakafuni pande zote mbili.  Wagonjwa wenye hali mbaya: wengine wana damu za masiku na mengineyo ya kibinadamu (sina haja ya kuyataja hapa, nadhani mnaelewa ninachozungumzia).

MaDr hawapiti ipasavyo.  Pengine hiyo hali ya wadini inawavunja moyo japo walikula kiapo cha kuwasaidia wagonjwa iwe itakavyokuwa.  Si kama ninawatetea, wao ndio wangekuwa wa kwanza kuleta mabadiliko, kuleta vurugu ili hali ya wadi na wagonjwa iboreshwe.  Kufikisha malalamiko wizarani.  Waziri wa afya ana hii habari?  Hata yupo?
MaNurse na wenyewe kwa ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi yao, hawafanyi kitu, hata wito hawana.

Mikojo na mengineyo vipo sakafuni kati ya wagonjwa.  MaNurse watapita kukusanya kusanya na kusafisha kijuu juu dakika 30 kabla ya muda wa kuwatembelea wagonjwa hujafika.  Muda mwingine wote sakafu ni chafu na mambo yote hayo.  MaNurse hawana nafasi ya kutosha kusema watapiga deki kona hadi kona kwa sababu wadi ipo imefura na wagonjwa hadi sakafuni.  Harufu hewani ni mbaya sana hata sijui wagonjwa wataponaje.
Mgonjwa anakalishwa na uchafu wake kwa muda mrefu sana.  Yaani utu na heshima (dignity) yake yote inadhalilishwa.

Vyandarua hamna.  Ukitaka chandarua, ni cha mission.  Ukitaka wakufungie cha kwako toka nyumbani, ni mission pia.
Wasafishaji na wenyewe wanadharau wagonjwa.  Kusafisha madirisha wanatumia mpira wa maji uliotoboka toboka.  Bomba la maji ni la bafuni hapo wadini.  Wanavuta huo mpira toka bombani hadi nje ubarazani, huku mpira unawapitia wagonjwa waliolala sakafuni na kuwalowesha.  Roho gani hii? Ni utu kweli?

Ninakuombeni
1. Nenda ukajionee, tuma mtu au mtu yeyote mwenye kusoma hii post akajionee. 
2. ui-post hili lalamiko langu "pengine" litaweza kuleta majadiliano ya mabadiliko.  Tusione kitu hakifanyi kazi kabisa tukakaa kimya. 
Maendeleo sio magari na manyumba, sehemu za starehe na vivalo vya nguvu.  Maendeleo ni huduma za afya, usafiri...sitaki nianze kuzungumzia maji na umeme - hio itakuwa post nyingine.....:-\
 
Naomba ufuatilie hili lalamiko, kiubinadamu tu.  Kesho atakuwa ndugu yako kalazwa Sewa haji, sio kama ninakuombea iwe hivyo lakini.  Pengine hatulalamiki kwa sababu hatujui,  Mimi ninajua na nimeona, tusiwe wakimya hata kwenye haki zetu.
Ukae salama.

No comments: