ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 12, 2011

MAITI YAFUKULIWA...GPL

Na Haruni Sanchawa
KINDUMBWEDUMBWE kimeibuka katika makaburi ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam baada ya familia moja kuchukua maiti isiyo yao  na kwenda kuizika.

Maiti iliyochukuliwa ilikuwa  ya marehemu Robert Ngwaito (pichani) ambaye alikuwa Mkristo lakini cha ajabu waliochukua maiti hiyo walidhani ni ya Said Mustafa na kulazimika kuizika Kiislamu katika makaburi hayo.

Aidha, habari zinasema ndugu wa marehemu Robert walipofika katika Hospitali ya Mwananyamala tayari kwa kuchukua mwili ili kuusafirisha kwenda Dodoma kwa mazishi,  walikuta maiti haipo hivyo kwa kushirikiana na uongozi na wahudumu wa chumba cha maiti, walibaini kuwa imechukuliwa na ndugu wa marehemu Saidi.

Viongozi wa Hospitali ya Mwananyamala walishirikiana na ndugu wa marehemu Robert na kwenda kuufukua mwili huo ili ukazikwe tena huko mkoani Dodoma.

Baba wa maiti iliyoachwa, Mzee Mustafa Abdallah, aliliambia gazeti hili kuwa  kidini ni makosa makubwa yamefanyika lakini hawana jinsi kwa sababu kila mtu anataka mtu wake akazikwe kwa imani yake ya dini, na kwa hilo wa kumlaumu ni yule aliyeenda kuutambua mwili huo.

Maiti iliyofukuliwa  ilisafirishwa usiku kwenda Dodoma, eneo la Mvumi Mission, kwa mazishi usiku
ambapo marehemu Said alizikwa siku iliyofuata  katika kaburi lilelile lililofukuliwa

No comments: