ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 12, 2011

Wafanyakazi Coca Cola Kwanza wagoma Dar

Wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha soda cha Coca Cola Kwanza, kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, wakiwa katika mgomo wao leo asubuhi. Wafanyakazi hao waligoma wakishinikiza uongozi wa Kiwanda hicho uwaongezee mishahara.





Baadhi ya wafanyakazi wakiongea na waandishi wa habari.


Kiongozi wa TUICO alifika kuwatuliza wafanyakazi hao na kuahidi kuzungumza naMenejimenti ya Kiwanda hicho. Mpaka kamera ya mjengwablog inaondoka eneo la Kiwanda hicho majira ya saa sita mchana, mgomo ulikuwa unaendelea na Uongozi wa kiwanda hicho ulikataa kuzungumza chochote na waandishi wa habari. Picha zote na Victor Makinda na kwa hisani ya Mjengwa BLOG

No comments: