pichani juu ni mamodo wa Anna katika pozi na chini ni Mtangazaji na Modo Jestina akionyesha mitindo ya mavazi kutoka kwa mbunifu Anna Lukindo.
Juu na chini ni Mamodels wakipita mbele ya watazamaji wakionyesha mitindo iliyobuniwa na mbunifu Mtanzania,Anna Lukindo
MC akitangaza jamabo kwenye onyesho hilo la mavazi
Mama Balozi pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi wetu Uingereza nao walikuwepo kummpa Tafu Mbunifu wa Mavazi Mtanzania,Anna Lukindo
Kutoka kushoto: Marium Kilumanga, Jestina George, Anna Shelukindo na mdau wakipata U-kodak Moment
Sheikh akimpa hongera Ann pamoja na Naibu balozi Chabaka
Mtanzania mbunifu wa mitindo ya nguo, Anna Lukindo, ametikisa ulimwengu wa fashion jijini london wikiendi iliopita. Anna alionyesha mavazi aliyobuni kwenye maonyesho ya La Geneve North Event, yaliyofanyika London siku ya Ijumaa tarehe 8.7.11 Ubunifu wa Anna ulipokelewa kwa vifijo na nderemo kwani ulikuwa ndio uliotia fora.
Kulikuwa na wabunifu wengine kumi, lakini Anna ndiye alikuwa mwafrika na Mtanzania pekee ambaye mavazi yake yalikubalika na kupendwa na watu wengi zaidi.
Mojawapo ya wageni na wadau mbalimbali walijjitokeza kumpa sapoti Anna ni Mh. Balozi wetu Peter Kallaghe na Mama Balozi, Naibu Balozi Chabaka Kilumanga pamoja na watanzania wengine.
Kwa niaba ya URBAN PULSE, tunapenda Kumpongeza Dada yetu Anna Na Kumtakia kila la kheri pamoja na Mafaniko Mema.
Kwa mawasiliano zaidi na Anna tembelea
Kwa mawasiliano zaidi na Anna tembelea
Pr/Media:Pauladpope@yahoo.co.uk
Web:www.annaluks.com
Twitter:@AnnaLukindo
imeletwa kwenu na:
URBAN PULSE CREATIVE
Urbanpulsecreative@googlemail.com
No comments:
Post a Comment